Uturuki : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Badiliko: arz:توركيا
d roboti Nyongeza: ee:Turkey
Mstari 140: Mstari 140:
[[dsb:Turkojska]]
[[dsb:Turkojska]]
[[dv:ތުރުކީވިލާތް]]
[[dv:ތުރުކީވިލާތް]]
[[ee:Turkey]]
[[el:Τουρκία]]
[[el:Τουρκία]]
[[en:Turkey]]
[[en:Turkey]]

Pitio la 15:52, 24 Machi 2009

Ramani ya Uturuki
Uturuki


Uturuki (Jamhuri ya Uturuki; Kituruki: Türkiye Cumhuriyeti) ni nchi ya kimabara ya Asia na Ulaya.

Sehemu kubwa iko Asia ya magharibi lakini sehemu ndogo ya eneo lake upande wa magharibi ya Bosporus iko Ulaya.

Eneo

Sehemu kubwa ya mipaka yake ni bahari: Mediteranea upande wa magharibi na kusini na Bahari Nyeusi upande wa kaskazini. Kwenye nchi kavi imepakana na Ugiriki na Bulgaria upande wa magharibi, Kaskazini-mashariki na Georgia, Armenia na Azerbaijan, kwa upande wa mashariki na Iran na upande wa kusini na Iraq na Syria.

Sehemu kubwa ya eneo lake ni Anatolia inayoonakana kama rasi kubwa kati ya Mediteranea na Bahari Nyeusi. Hali ya nchi ndani ya Anatolia mara nyingi ni yabisi na kilimo kinategemea umwagiliaji. Safu za milima inafuatana na pwani za kusini na kaskazini. Sehemu ya mashariki ya nchi kuelekea Uajemi na Kaukazi ina milima mingi.

Maeneo ya pwani yanapokea mvua na huwa na rutba.


Wakazi

Uturuki ina wakazi milioni 69. Wengi wao ni Waturuki.

Katika mashariki ya Uturuki watu wengi ni Wakurdi ambao ni milioni 14 au takriban 20%-25% za raia wote wa Uturuki.

Kuna mabaki madogo tu ya Wagiriki na Waarmenia waliowahi kukalia sehemu kubwa za nchi hadi mwisho wa milki ya Osmani. Kwenye maeneo jirani na Syria wako pia Waarabu.

Kutokea kwa Uturuki ya kisasa

Uturuki ya kisasa ietokea kama nchi ya pekee baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia. Waturuki waliwahi kuwa kiini cha Milki ya Osmani iliyounganisha mataifa mengi chini ya Sultani wa Konstantinopoli.

Jamhuri ya Uturuki ilianzishwa mwaka 1923 na jenerali Kemal Atatürk baada ya vita mbili. Vita ya kwanza ilikuwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia iliyovunja Milki ya Osmani, na vita ya pili ilifuata wa kuondoa wanajeshi wa Ugiriki na nchi nyingine zilizowahi kuingia ndani sehemu niliyokuwa imebaki baada ya kuvinjika kwa dola kubwa.

Atatürk alileta mabadiliko mengi yaliyolenga kuondoa utamaduni wa kale wa Waosmani na enzi za utawala wa sultani wa Kiislamu. Magharibi ya nchi imeendelea sana lakini katika maeneo ya mashariki yamebaki nyuma.

Nchi ya kisasa

Siku hizi Uturuki inalenga kuingia katika Umoja wa Ulaya.

Serikali ina utaratibu wa kidemokrasia ya vyama vingi. Utawala wa nchi ni kwa mikoa 81.

Mji mkuu ni Ankara iliyoko katika kitovu cha Anatolia. Mji mkubwa ni Istanbul iliyoitwa zamani Konstantinopoli na zamani zaidi Bizanti iliyokuwa mji mkuu wa Dola la Uturuki hadi 1923.

Picha za Uturuki


Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA