Pamukkale

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chemchemi za moto za Pamukkale
Ukuta mweusi wa chokaa

Pamukkale (Kituruki: Boma la pamba) ni kijiji katika Uturuki wa Kusini-Magharibi pamoja na maajabu asilia inayohesabiwa kwenye mahali pa urithi wa dunia.

Maajabu ya Pamukkale ni maporomoko ya maji ya moto yenye kiwango kikubwa cha chumvi ya chokaa. Chokaa hiki kiliganda kwa karne nyingi ikajenga ngazi za rangi nyeupe zinazovuta watalii wengi.

Maghofu ya mji wa kale wa Hierapoli ni karibu na kijiji cha leo.

Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Pamukkale kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.