Hierapoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa maigizo wa Hierapoli ya kale
Kaburi la Mtume Filipo.

Hierapoli ilikuwa mji wa ustaarabu wa Ugiriki ya Kale katika Asia Ndogo (Uturuki wa leo).

Maghofu yake yako karibu na maji ya moto ya Pamukkale. Hierapoli pamoja na Pamukkale huhesabiwa kati ya mahali pa urithi wa dunia.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mji ulianzishwa mahali pake kwa sababu ya chemchemi za moto ukakua tangu karne ya 3 KK.

Mwandishi wa habari za mianzo ya Biblia Papias wa Hierapoli alikuwa askofu wa mji huo katika karne ya 2 akaandika kwamba huko ndiko Mtume Filipo alikoinjilisha pamoja na mabinti wake watatu hadi kifo chake (80 hivi).

Waraka kwa Wakolosai ulitaja tayari jumuia ya Kikristo ya mji huo (4:13).

Ukaendelea hadi nyakati za vita za misalaba ambapo ulishambuliwa na kuharibiwa mara kadhaa.

Baada ya uangamizi uliosababishwa na tetemeko la ardhi mwaka 1334 ukaachwa na mahali pake hapajakaliwa tena.

Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hierapoli kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.