Nenda kwa yaliyomo

Papias

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Papias

Papias (70 hivi - 155 hivi) alikuwa mfuasi wa Mtume Yohane pamoja na Polikarpo.

Baadaye akawa askofu au kiongozi wa ushirika wa Kikristo mjini Hierapoli (karibu na Pamukkale ya leo katika Uturuki).

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Februari[1].

Maandishi[hariri | hariri chanzo]

Papias ni maarufu katika historia ya Ukristo kwa sababu ni mtu wa kwanza anayejulikana kukusanya habari juu ya waandishi wa Agano Jipya. Aliandika habari hizo katika vitabu vitano vilivyoitwa "Maelezo kuhusu maneno ya Bwana (Yesu)".

Maandiko hayo yamepotea lakini sehemu za yaliyomo yake zimehifadhiwa katika vitabu vingine vya Irenaeus wa Lyons ("Dhidi ya uzushi") na Eusebi wa Kaisarea ambao walikuwa na vitabu vyake wakati wa kuandika vya kwao.

Papias alimtaja Mtume Mathayo kama mwandishi wa Injili ya Mathayo na "Presbiteri Marko mfasiri wa Petro" kama mwandishi wa Injili ya Marko.

Waandishi wa baadaye katika Ukristo wa kale hawakukubaliana juu yake. Wengine walimsifu, wengine walimwona kama mtu asiye na habari za maana.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.