Mtakatifu Marko
Mtakatifu Marko (kwa Kilatini Mārcus; kwa Kigiriki Μᾶρκος) aliishi katika karne ya 1 BK. Alikuwa Myahudi wa Yerusalemu aliyeongokea mapema Ukristo pamoja na Maria mama yake. Kanisa la kwanza lilikuwa linakusanyika nyumbani mwao.
Alifanya kazi na mitume Paulo na Barnaba katika kuhubiri Injili huko Kupro na Uturuki wa leo.
Baadaye alikuwa na Mtume Petro na Paulo katika mji wa Roma hadi walipouawa na serikali ya Kaisari Nero (dhuluma ya miaka 64-68).
Ndipo, kwa kufuata mafundisho ya Petro aliyemwita mwanae, alipoamua kuandika Injili ya kwanza, iliyotumiwa na kufuatwa na Mtume Mathayo na Mwinjili Luka, ingawa katika orodha za Biblia inashika nafasi ya pili.
Kadiri ya mapokeo alifariki wakati akifanya kazi ya kuanzisha Kanisa huko Aleksandria nchini Misri.
Tangu kale anaheshimiwa na madhehebu mengi ya Ukristo kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 25 Aprili[1].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- "The Apostle and Evangelist Mark (40–62)". Official web site of the Greek Orthodox Patriarchate of Alexandria and All Africa. Iliwekwa mnamo 2011-02-07.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- The Life, Miracles and Martyrdom of St. Mark the Evangelist of Jesus Christ Archived 4 Oktoba 2015 at the Wayback Machine.
- H.B. Swete, 'St. Mark in the New Testament'
- H.B. Swete, 'St. Mark in Early Tradition'
- St. Mark the Apostle, Evangelist, and Preacher of the Christian Faith in Africa
- Joseph MacRory (1913). "St. Mark". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company.
- Apostle Mark the Evangelist of the Seventy Orthodox icon and synaxarion
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtakatifu Marko kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |