Nenda kwa yaliyomo

Mtakatifu Marko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtakatifu Marko
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho   Utoto wa Yesu   Ubatizo   Arusi ya Kana   Utume wa Yesu   Mifano ya Yesu   Miujiza ya Yesu   Kugeuka sura   Karamu ya mwisho   Msalaba wa Yesu   Maneno saba   Kifo cha Yesu   Ufufuko wa Yesu   Kupaa mbinguni   Ujio wa pili  Yesu na matabiri ya Agano la Kale   Injili   Majina ya Yesu katika Agano Jipya   Yesu kadiri ya historia   Tarehe za maisha ya Yesu   Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi   Kiaramu   Bikira Maria   Yosefu (mume wa Maria)   Familia takatifu   Ukoo wa Yesu   Ndugu wa Yesu   Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya  · Mitazamo ya Kikristo   Mitazamo ya Kiyahudi   Mitazamo ya Kiislamu   Yesu katika sanaa

Mtakatifu Marko (kwa Kilatini Mārcus; kwa Kigiriki Μᾶρκος; aliishi katika karne ya 1 BK) alikuwa Myahudi wa Yerusalemu aliyeongokea mapema Ukristo pamoja na Maria mama yake. Kanisa la kwanza lilikuwa linakusanyika nyumbani mwao.

Alifanya kazi na mitume Paulo na Barnaba katika kuhubiri Injili huko Kupro na Uturuki wa leo.

Baadaye alikuwa na Mtume Petro na Paulo katika mji wa Roma hadi walipouawa na serikali ya Kaisari Nero (dhuluma ya miaka 64-68).

Ndipo, kwa kufuata mafundisho ya Petro aliyemwita mwanae, alipoamua kuandika Injili ya kwanza, iliyotumiwa na kufuatwa na Mtume Mathayo na Mwinjili Luka, ingawa katika orodha za Biblia inashika nafasi ya pili.

Kadiri ya mapokeo alifariki wakati akifanya kazi ya kuanzisha Kanisa huko Aleksandria nchini Misri [1].

Tangu kale anaheshimiwa na madhehebu mengi ya Ukristo kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 25 Aprili[2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Marejeo ya Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 144
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 123-124
  • Maurice Soseleje, Kalendari yetu – Maisha ya Watakatifu – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1986 – ISBN 9976-63-112-X, uk. 37-38

Marejeo ya lugha nyingine

[hariri | hariri chanzo]
  • "The Apostle and Evangelist Mark (40–62)". Official web site of the Greek Orthodox Patriarchate of Alexandria and All Africa. Iliwekwa mnamo 2011-02-07.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtakatifu Marko kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.