Nenda kwa yaliyomo

Papa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mapapa)
Kwa samaki anayeitwa kwa Kiswahili "papa" tazama papa (samaki)
Papa Pius IX, alishika cheo hicho kwa muda mrefu kuliko wote (1846-1878).
Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria

Muundo

Papa: Fransisko
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Liturujia ya Trento Milano Toledo Braga Lyon Canterbury)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Papa (neno la mkopo kutoka Kilatini lakini lenye asili ya Kigiriki, πάππας, pappas,[1] jina ambalo mtoto anamuitia baba yake)[2]ni cheo cha kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kote. Cheo hicho kinategemea kile cha askofu wa Roma.[3]

Kiasili neno la Kilatini "Papa" linamaanisha "Baba", nalo likawa cheo kutokana na nia ya kumtaja askofu wa Roma kwa heshima ya pekee. Msingi wa heshima hiyo ni imani ya Wakatoliki kuwa askofu wa Roma ni mwandamizi wa Petro, mkuu wa mitume wa Yesu.

Wakatoliki huamini ya kwamba Petro alipewa na Yesu kazi ya kuongoza Kanisa lote kwa niaba yake na ya kwamba jukumu hilo linaendelea kati ya waandamizi wa Petro kwenye kiti cha askofu wa Roma ambacho kwa heshima kinaitwa Ukulu mtakatifu.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Upapa ni kati ya vyeo vya zamani zaidi duniani na umeathiri sana historia ya binadamu kwa miaka karibu 2000.[4]Athari hiyo iliweza kuwa nzuri au mbaya, kadiri ya matendo ya mhusika.[5][6][7]

Kwa muda mrefu mamlaka ya Papa upande wa siasa, hasa juu ya mikoa ya Italia ya Kati, ilisababisha nchi nyingine na koo tajiri za Roma zijiingize katika uchaguzi ili kupitisha watu wao, hata wasiofaa. Upande mwingine, Mapapa waliathiriwa na utamaduni na mazingira ya nyakati zao, hasa tapo la Renaissance, kiasi cha kuzama katika anasa.

Baada ya Dola la Papa kutekwa na Ufalme wa Italia (1860-1870), Mapapa wameweza kushughulikia zaidi mambo ya kiroho na kujitokeza kwa ubora.[8][9]Kwa miaka ya karibuni inatosha kumfikiria Papa Yohane Paulo II na mchango wake katika kuangusha ukomunisti katika Ulaya Mashariki.

Majina ya mapapa

[hariri | hariri chanzo]
The signature of Pope Francis
Sahihi ya Papa Fransisko.

Papa huchaguliwa na makardinali wa Kanisa Katoliki baada ya mtangulizi wake kufa au kung'atuka. Baada ya kuchaguliwa papa mpya anaweza akajipatia jina jipya. Tangu tarehe 13 Machi 2013 ni Papa Fransisko, ambaye awali aliitwa Jorge Mario Bergoglio, kutoka Argentina.

Majina ya mapapa wengine wa Kanisa Katoliki yanapatikana katika orodha ya mapapa.

Mkuu wa Vatikano

[hariri | hariri chanzo]

Papa ni pia mkuu wa nchi huru ya Mji wa Vatikano iliyopo ndani ya mji wa Roma (ambao ni mji mkuu wa Italia).[10]

Cheo cha "Papa" penginepo

[hariri | hariri chanzo]

Cheo cha Papa hutumiwa pia na baadhi ya madhehebu mengine ya Kikristo kwa viongozi wao, hasa kwa mkuu wa Kanisa la Kikopti huko Misri.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "American Heritage Dictionary of the English Language". Education.yahoo.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-06. Iliwekwa mnamo 2010-08-11.
  2. "Liddell and Scott". Oxford University Press. Iliwekwa mnamo 2013-02-18.
  3. "Christ's Faithful - Hierarchy, Laity, Consecrated Life: The episcopal college and its head, the Pope". Catechism of the Catholic Church. Vatican City: Libreria Editrice Vaticana. 1993. Iliwekwa mnamo 14 Aprili 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Collins, Roger. Keepers of the keys of heaven: a history of the papacy. Introduction (One of the most enduring and influential of all human institutions, (...) No one who seeks to make sense of modern issues within Christendom - or, indeed, world history - can neglect the vital shaping role of the popes.) Basic Books. 2009. ISBN 978-0-465-01195-7.
  5. Faus, José Ignacio Gonzáles. "Autoridade da Verdade - Momentos Obscuros do Magistério Eclesiástico". Capítulo VIII: Os papas repartem terras - Pág.: 64-65 e Capítulo VI: O papa tem poder temporal absoluto – Pág.: 49-55. Edições Loyola. ISBN 85-15-01750-4. Embora Faus critique profundamente o poder temporal dos papas ("Mais uma vez isso salienta um dos maiores inconvenientes do status político dos sucessores de Pedro" - pág.: 64), ele também admite um papel secular positivo por parte dos papas ("Não podemos negar que intervenções papais desse gênero evitaram mais de uma guerra na Europa" - pág.: 65).
  6.  Jarrett, Bede (1913). "Papal Arbitration". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company.
  7. Such as regulating the colonization of the New World. See Treaty of Tordesillas and Inter caetera.
  8. História das Religiões. Crenças e práticas religiosas do século XII aos nossos dias. Grandes Livros da Religião. Editora Folio. 2008. Pág.: 89, 156-157. ISBN 978-84-413-2489-3
  9. "último Papa - Funções, eleição, o que representa, vestimentas, conclave, primeiro papa". Suapesquisa.com. Iliwekwa mnamo 2013-02-18.
  10. "Vatican City State - State and Government". Vaticanstate.va. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-07-22. Iliwekwa mnamo 2010-08-11. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
      .

Marejeo mengine

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.