Jamhuri ya Watu wa Zanzibar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Visiwa vya Zanzibar (Unguja na Pemba)
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
Bendera ya Zanzibar - tangu 2005
Lugha ya Taifa Kiswahili
Mji Mkuu Zanzibar
Rais Amani Abeid Karume
Eneo
121,320 km²
Wakazi
984,625
Dini Waislamu takriban 96-99%, Wakristo, Wahindu
Uhuru Kutoka Uingereza
  19.12.1963, Mapinduzi 12.01.1964
Fedha TSh
Visiwa vya Unguja na Pemba (ramani haionyeshi umbali kati ya visiwa hali halisi)

Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayojitawala katika mambo yake ya ndani. Eneo lake ni sawa na funguvisiwa ya Zanzibar iliyopo mbele ya mwambao wa Afrika ya Mashariki karibu na Tanganyika au Tanzania bara. Inajumuisha visiwa vikubwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogovidogo. Kwa jumla mikoa mitano ya Tanzania imo ndani ya Zanzibar ikiwa mitatu iko Unguja na miwili Pemba.

Zanzibar inatawaliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Raisi Amani Abeid Karume aliyekuwa mgombea wa CCM amechaguliwa mara ya pili na wananchi wote tar. 30.10. 2005 katika kura iliyopingwa na chama cha Upinzani CUF.

Zanzibar ina Bunge lake lenye wabunge 50 wanaochaguliwa kwa muda wa miaka mitano.

Mji mkuu na makao makuu ya serikali ni Jiji la Zanzibar ambalo liko kisiwa cha Unguja. Mji mkuu wa kisiwa cha Pemba ni Chake Chake. Idadi ya wakazi wote ilikuwa 984,625 mwaka 2002, wakiwa 622.459 wakazi wa Unguja na 362.168 wakazi wa Pemba.

Biashara ya Zanzibar ni kilimo na utalii. Mazao yanayouzwa nje ni hasa karafuu, basibasi, mdalasini na pilipili.

Jamhuri ya watu wa Zanzibar ilianzishwa baada ya mapinduzi ya 1964 iliyomaliza Usultani wa Zanzibar. Rais wa kwanza alikuwa Abeid Amani Karume hadi 1972 aliyefuatwa na Aboud Jumbe (1972-1984). Rais wa tatu aliyemfuata alikuwa Ali Hassan Mwinyi (1984-1995) aliyeendelea kuwa pia rais wa Tanzania tangu 1985.

Rais wa sasa ni Amani Abeid Karume ambaye ni mwana wa rais wa kwanza.

[hariri] Siasa

Zanzibar ina vyama vikuu vya kisiasa viwili,Chama tawala CCM na Chama cha wananchi CUF,tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vyama hivi vimekua vikivutana kaika mambo mbali mbali na kusababisa uchumi wa Zanzibar kuathirika sana kutokana na viongozi kujadili siasa katika vikao vya baraza la wawakilishi badala ya maslahi ya waliowachagua,tofauti sana na kwa upande wa Bara ambapo maendeleo mingi yamekua yakijionesha.

[hariri] Uchumi

Uchumi wa Zanzibar ni uchumi wa hali ya chini kabisa ambao mwananchi wa kawaida anaishi chini ya dola moja kwa siku au kutokua na uhakika wa kupata chochote. Hilo linatokana na viongozi wa vyama kutoonesha mori katika kutatua matatizo au kuweka mbinu za kuleta maendeleo,badala yake ni kujadili siasa kwa muda mwingi. Zanzibar ni nchi yenye matumaini katika uchumi lakini kutokana na migogoro ya kisiasa imekua katika hali duni kabisa,ni hivi majuzi tu balozi wa Marekani alisisitiza kuwa umuhimu wa kuwepo mashirikiano katika siasa ili kuiwezesha Zanzibar kuinuka katika hali ya kiuchumi.

[hariri] Viuongo vya nje


 
Mikoa ya Tanzania
Bandera Tanzania
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Iringa | Kagera | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |
World.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.