Bendera ya Zanzibar
bendera ya kale
bendera nyekundu sawa na Omani wakati ule,
kiasili ni bendera ya Sharifa wa Maka
Zanzibar ilhali ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipata tena bendera ya pekee tangu Januari 2005. Inaunganisha bendera ya Tanzania na ile ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ya mwaka 1964 iliyotumika kati ya mapinduzi ya Januari na muungano ya Zanzibar na Tanganyika katika Juni 1964.
Zanzibar ilikuwa na bendera yake tangu kuhamia kwa Sultani wa Omani kutoka Maskat kuja Zanzibar. Bendera nyekundu ilikuwa sawa na ile ya Sharifa wa Maka.
Baada ya kupata uhuru mwaka 1963 usultani uliongeza alama ya karafuu katika bendera yake.
Viungo vya nje [hariri]
| Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
|
||||||||||||||