Zanzibar (Jiji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Jiji la Zanzibar)


Jiji la Zanzibar
Jiji la Zanzibar is located in Tanzania
Jiji la Zanzibar
Jiji la Zanzibar

Mahali pa mji wa Zanzibar katika Tanzania

Majiranukta: 6°9′36″S 39°12′0″E / 6.16000°S 39.20000°E / -6.16000; 39.20000
Nchi Tanzania
Mkoa Unguja Mjini Magharibi
Wilaya Unguja Mjini
Beit-al-Ajaib, yaani Jumba la Maajabu (1907).

Jiji la Zanzibar ni mji mkubwa wa kisiwa cha Unguja na mji mkuu wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Pia ni wilaya katika Mkoa wa Unguja Mjini Magharibi wa Tanzania.

Jiji lina wakazi 206,292 (sensa ya mwaka 2002).[1]

Jina[hariri | hariri chanzo]

Mji Mkongwe[hariri | hariri chanzo]

Kitovu cha historia yake ni Mji Mkongwe (Stone Town) ulioandikishwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia" (World Heritage).

Nyumba za Mji Mkongwe zilijengwa tangu mwaka 1830 wakati Sultani Sayyid Said alipohamisha mji mkuu wake kutoka Omani kuja Unguja.

Kati ya majengo maarufu ni Beit al Ajaib (yaani Jumba la Maajabu lililobomoka tarehe 24 Desemba 2020[2]), boma la kale, Kanisa Kuu la Kianglikana lililojengwa mahali pa soko la watumwa na hasa nyumba nyingi za kihistoria za ghorofa zilizojengwa na famila za tabaka la matajiri Waarabu zenye milango yenye mapambo mazuri.

Mji Mkongwe unapokea watalii wengi kila mwaka.

Mji wa kisasa umekua sana ng'ambo ya Mji Mkongwe.

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Stone Town travel guide kutoka Wikisafiri

Kata za Wilaya ya Mjini Unguja - Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja - Tanzania

Amani | Banko | Chumbuni | Gulioni | Jang'ombe | Karakana | Kidongo Chekundu | Kikwajuni Bondeni | Kikwajuni Juu | Kilimahewa Bondeni | Kilimahewa Juu | Kilimani | Kiponda | Kisimamajongoo | Kisiwandui | Kwaalimsha | Kwaalinatu | Kwabintiamrani | Kwahani | Kwamtipura | Kwamtumwajeni | Kwa Wazee | Magomeni | Makadara | Malindi | Mapinduzi | Maruhubi | Masumbani | Matarumbeta | Mboriborini | Mchangani | Meya | Miembeni | Migombani | Mikunguni | Mitiulaya | Mkele | Mkunazini | Mlandege | Mnazimmoja | Mpendae | Muembeshauri | Muungano | Mwembeladu | MwembeMadema | Mwembemakumbi | Mwembetanga | Nyerere | Rahaleo | Saateni | Sebleni | Shangani | Shaurimoyo | Sogea | Urusi | Vikokotoni


Makala hii kuhusu maeneo ya Unguja bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Zanzibar (Jiji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.