Nenda kwa yaliyomo

Omani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Waomani)
سلطنة عُمان
Sulṭanat ʿUmān

Usultani wa Omani
Bendera ya Omani Nembo ya Omani
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: (hakuna)
Wimbo wa taifa: Nashid as-Salaam as-Sultani
Lokeshen ya Omani
Mji mkuu Maskat
23°61′ N 58°54′ E
Mji mkubwa nchini Muskat
Lugha rasmi Kiarabu
Serikali Ufalme
Haitham bin Tariq Al Said
{{{sovereignty_type}}}
Waosmani kufukuzwa
1741
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
309,500 km² (ya 70)
(kidogo sana)
Idadi ya watu
 - Julai 2019 kadirio
 - 2010 sensa
 - Msongamano wa watu
 
4,975,0001 (ya 129)
2,773,479
13/km² (ya 216)
Fedha Rial (OMR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+4)
(UTC+4)
Intaneti TLD .om
Kodi ya simu +968

-

1Ndani ya idadi ya wakazi kuna watu 577,293 wasio raia



Ramani ya Omani

Usultani wa Omani (kwa Kiarabu:سلطنة عُمان Saltanat ˤUmān) ni nchi ya Bara Arabu katika Asia ya Magharibi.

Imepakana na Maungano ya Falme za Kiarabu, Saudia na Yemen, halafu Bahari Hindi na Ghuba ya Omani.

Utawala wa nchi hufuata muundo wa kifalme usiobanwa na masharti ya katiba.

Mji mkuu ni Maskat (Omani).

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Omani imekaliwa na watu kwa zaidi ya miaka 100,000.

Omani ilikuwa kituo muhimu cha biashara kwenye Bahari Hindi na Ghuba ya Uajemi tangu milenia mbili KK.

Athira za nje

[hariri | hariri chanzo]

Tangu kuja kwa Uislamu Omani ilikuwa ama chini ya Uajemi au chini ya khalifa wa Baghdad na baadaye Dola la Seljuki.

Kati ya miaka 1507 na 1650 mji wa Maskat na pwani ya Omani vilitawaliwa na Ureno.

Makabila ya bara yaliunganika chini ya maimamu wa madhehebu ya Kiislamu ya Waibadiya na Imam Nasir ibn Murshid († 1649) alifaulu kupunguza eneo la Wareno. Mfuasi wake Sultan ibn Saif aliwafukuzwa kabisa Wareno na kushambulia vituo vyao kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki.

Omani na Afrika ya Mashariki

[hariri | hariri chanzo]

Masultani wa Omani walitawala pwani ya Afrika ya Mashariki katika karne ya 19. Mwaka 1830 Sultani Sayyid Said alihamisha mji mkuu wake kutoka Omani kuja mji wa Zanzibar (Unguja). Baada ya kifo chake mwaka 1856 dola liligawiwa kuwa nchi mbili:

Maskat na Omani

[hariri | hariri chanzo]

Tangu mwaka 1891 sultani alikuwa kabisa chini ya mamlaka ya mwakilishi Mwingereza hata kama kwa jina nchi haikuwa koloni. Kati ya makabila ya Omani bara ulikua upinzani dhidi ya utawala wa Sultani mjini Maskat na athira kubwa ya Uingereza katika serikali yake. Hali halisi kanda ya pwani ilikuwa chini ya sultani wa Maskat lakini katika sehemu za ndani, yaani Oman yenyewe, makabila yalijitawala au kuungana kumchagua imamu kama mkuu wao wa pamoja. Kwenye mwezi wa Mei mwaka 1913 viongozi wa makabila ya ndani pamoja na vongozi wa dini walikutana wakamchagua tena imamu.

Baada ya vita ya miaka 7 pande mbili zilipatana mwaka 1920 kugawa nchi: upande wa imamu ulikubali kutoshambulia tena miji ya vijiji vya pwani, sultani alikubali kuheshimu hali ya kujitawala ya maeneo ya ndani chini ya imamu[1]. Sehemu za ndani ziliendelea kujitawala chini ya imamu hadi mwaka 1954.

Maungano chini ya Sultani Taimur

[hariri | hariri chanzo]

Amani ilivunjwa mwaka 1954 wakati Sultani Said bin Taimur alitoa kibali kwa kampuni ya Kiingereza kutafuta mafuta ya petroli katika maeneo ya imamu. Kuingia kwa kikosi cha sultani kilichoongozwa na maafisa Waingereza kulikuwa chanzo cha vita iliyoendelea kwa miaka 5 hadi ushindi wa upande wa sultani aliyepata usaidizi wa jeshi la Uingereza. Hivyo Maskat na Omani iliunganishwa kwa nguvu ya kijeshi.

Sultani Said bin Taimur alipeleka mji mkuu wake kwenda Salalah akaendelea kutawala kutoka pale. Said bin Taimur alianza utawala wake akirithi madeni makubwa akalenga kumaliza deni na kutoingia madeni mapya. Hivyo alikataa uwekezaji katika miundombinu kama vile barabara au taasisi za elimu na afya. Hadi mwaka 1970 Omani ilikuwa na kilomita tu 10 za barabara za lami, hospitali 1 pekee na shule 3. Matumizi ya baisikeli na miwani ya Jua yalikatazwa na hapakuwa na simu kwa raia binafsi. Mageti ya miji iliyozungukwa bado na kuta zilifungwa wakati wa machweo. Wakati wa usiku kila raia alitakiwa kutembea akishika koroboi. Sultani mwenyewe aliangalia maombi yote ya viza kwa wageni waliotaka kuingia nchini, na vilevile vibali kwa wananchi waliotaka kutoka nje ya nchi.

Mapinduzi ya Qabus

[hariri | hariri chanzo]

Kuanzia mwaka 1965 kulitokea uasi katika jimbo la Dhofar uliopanuka kati ya makabila ya milimani ukiongozwa na wanamapinduzi Wakomunisti kutoka nchi jirani ya Yemen Kusini. Jeshi la sultani lililoongozwa na maafisa Waingereza lilipambana na uasi huu na Waingereza walielewa kwamba sultani Taimur hakuwa na siasa ya kukomesha uasi. Hapo waliandaa mapinduzi ya kijeshi baada ya kuwasiliana na Qaboos bin Said al Said mwana pekee wa Taimur aliyewahi kusoma Uingereza lakini baada ya kurudi aliwekwa na baba yake chini ya ulinzi ndani ya kasri ya kifalme. Tarehe 23 Julai 1970 wanajeshi chini ya Waingereza walimkamata sultani Taimur aliyepelekwa mara moja uhamishoni Uingereza, Qabus alitangazwa kuwa sultani mpya.

Mabadiliko chini ya Qabus

[hariri | hariri chanzo]

Tangu 1970 hadi 2019 Omani ilitawaliwa na sultani Qabus aliyeanzisha mara moja mabadiliko mengi ya kuifanya kuwa nchi ya kisasa. Utumwa ulifutwa na mapato ya serikali, pamoja na hazina ya sultani, vilitumiwa kuwekeza katika miundombinu, ujenzi wa barabara, shule na hospitali. Vijana walitumwa ng'ambo ili wasome elimu ya kisasa.

Tangu miaka ya 1980, uwekezaji umelenga zaidi upande wa kuanzisha viwanda na kuanzisha kilimo cha kisasa ilhali nchi iliendelea kutegemea mapato ya uuzaji wa mafuta. Katika miaka 50 ya utawala wake nchi ilisogea mbele na mapato ya wananchi yaliongezeka mara 50.

Wakazi wengi ni Waarabu, Wabaluchi, Wahindi, Waafrika n.k. Zaidi ya asilimia 40 ni wahamiaji.

Wenyeji karibu wote ni Waislamu, wakati wageni ni wa dini tofautitofauti. Kwa jumla Waislamu ni 85.9%, Wakristo 6.5%, Mabanyani 5.5% n.k.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kiarabu, lakini Kiingereza, Kibaluchi, Kiurdu na Kiswahili pia vinatumika sana.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Jeremy Jones, Nicholas Ridout: A History of Modern Oman, uk. 91, Cambridge University Press, 2015 (google books)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Omani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.