Bikira Maria wa Fatima

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu iliyotiwa taji ya Bikira Maria ya Fatima katika kikanisa kilichopo mahali pa njozi.
Mahali pa Fatima nchini Ureno.

Bikira Maria wa Fatima (jina rasmi: Bibi Yetu wa Rosari wa Fatima; kwa Kireno: Nossa Senhora do Rosário de Fátima) ni jina mojawapo la Bikira Maria lililotokana na njozi maarufu za mwaka 1917 walizozisimulia watoto watatu wa Fatima, Ureno: Lusia Santos na binamu zake Yasinta Marto na Fransisko Marto.

Njozi hizo zilithibitishwa na Kanisa Katoliki kuwa za kuaminika[1], hata ikaanzishwa kumbukumbu yake katika liturujia kila mwaka katika tarehe ya ile ya kwanza, 13 Mei[2].

Tarehe 13 Mei 1946, Papa Pius XII alikubali rasmi sanamu iliyotengenezwa kutokana na masimulizi hayo itiwe taji. Tarehe 11 Novemba 1954, alitangaza patakatifu pa Fatima kuwa basilika kwa hati Lucer Superna.

Umati wa waumini wanaohiji huko ili kukazia macho ya imani huyo Mama mwema sana kadiri ya neema ya Mungu aliyojaliwa, anayeaminika kushughulikia daima matatizo ya watu, unavutiwa kuongoka na kuombea wakosefu.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bikira Maria wa Fatima kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.