Nenda kwa yaliyomo

Australia na Pasifiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Australia na Visiwa vya Pasifiki
* AS: Samoa ya Marekani * AU: Australia * CK: Visiwa vya Cook * FJ: Fiji * FM: Mikronesia * GU: Guam (USA) * KI: Kiribati * MH: Visiwa vya Marshall * MP: Visiwa vya Mariana * NC: Kaledonia Mpya (Ufaransa) * NR: Nauru * NU: Niue (New Zealand) * NZ: New Zealand * PF: Polynesia ya Kifaransa * PG: Papua Guinea Mpya * PN: Pitcairn (Uingereza) * PW: Palau * SB: Visiwa vya Solomon * TL: Timor ya Mashariki * TK: Tokelau * TO: Tonga * TV: Tuvalu * US: Hawaii * VU: Vanuatu * WF: Wallis na Futuna (Ufaransa) * WS: Samoa ya Magharibi Nchi za Asia * [BN]: Brunei * [CN]: China * [ID]: Indonesia * [MY]: Malaysia * [PH]: Ufilipino * [TW]: Taiwan

Australia na Visiwa vya Pasifiki (pia: Oceania, Okeania, Oshania) hujumlishwa mara nyingi pamoja katika hesabu ya mabara.

Hasa watu kwenye visiwa vingi vya Pasifiki wana utamaduni wa karibu. Vilevile historia ya visiwa hivyo kabla ya kuenea kwa ukoloni imefanana katika mengi.

Bara au la?

[hariri | hariri chanzo]

Hivyo mara nyingi sehemu hii ya dunia imeitwa "Bara la Kiutamaduni". Jina hili si sahihi kijiografia kwa sababu maeneo yake yako juu ya mabamba ya gandunia tofauti, kama vile bamba la Pasifiki, bamba la Australia na mengine madogo. Hata wataalamu hawapatani kuhusu mipaka ya eneo hilo.

Kwa lugha nyingi za dunia jina la "Oceania" (Okeania, Oshania) limekuwa la kawaida kutokana na neno la Kigiriki "okeanos" (kwa Kilatini: oceanus; kwa Kiingereza: ocean). Hivyo "Oceania" yamaanisha "nchi katika bahari". Ila tu hatuoni faida ya kuingiza neno hili katika lugha ya Kiswahili kwa sababu ni neno lisiloeleweka vizuri. Mara wataalamu hujadili "Oceania" kuwa visiwa vya Pasifiki pamoja na Australia; mara wanaona "Oceania" ni visiwa vile pekee bila Australia na wengine wanasema wenyewe "visiwa vya Pasifiki" ingekuwa jina zuri zaidi kama Australia haihesabiwi.

"Australasia" imekuwa jaribio tofauti la kutaja eneo, hasa kati ya wataalamu wa Australia, ila tu halipendwi na watu wengi visiwani. Hivyo imetumiwa zaidi kwa kanda la Australia na visiwa jirani pekee.

Visiwa vyote kwa pamoja (bila Australia yenyewe) hukadiriwa kuwa 7,500 vyenye eneo la nchi kavu la kilomita za mraba milioni 1.3 vilivyosambaa katika eneo la bahari la kilomita za mraba milioni 70. Takriban visiwa 2,100 vimekaliwa na watu milioni 14.9.

Jiolojia

[hariri | hariri chanzo]

Eneo hili si bara kwa maana ya jiolojia. Visiwa vikubwa vya New Zealand, Guinea Mpya, Kaledonia Mpya na Tasmania ni mabaki ya bamba la Gondwana ya kihistoria. Guinea Mpya imetenganishwa na Australia kwa bahari ya Arafura isiyo na kina kirefu na wakati wa enzi ya barafu iliyopita zilikuwa kama nchi moja kwa sababu uwiano wa bahari ulikuwa chini kuliko leo.

Visiwa vingi katika Pasifiki ni milima ya volkeno inayoinuka kutoka tako la bahari hadi uso wa maji; mara nyingi zinaonyesha kasoko. Visiwa vingine vinajengwa na matumbawe yanayokua juu ya volkeno ambazo zimeishia kidogo chini ya uso wa bahari. Visiwa vingine ni atoli ambako matumbawe yamejenga tuta tumbawe kwa umbo la mviringo kuzunguka kisiwa cha kivolkeno.

Sababu ya kutokea kwa volkeno nyingi ni miendo ya gandunia katika tabaka za ganda la dunia chini ya bahari. Ngozi ya nje au ganda la dunia hufanywa na vipande mbamlimbali (=mabamba ya gandunia) vinavyoelea juu ya tabaka ya mwamba moto na kiowevu. Pale ambako vipande hivi vinagusana mara kwa joto na mwamba moto ulioyeyuka unapanda juu; pale ambao kupanda huku kunatokea haraka tunaona volkeno na hivyo kisiwa kipya kutokea. Mfano ni safu ya visiwa vya Hawaii ambavyo ni safu ya milima ya volkeno inayoanza kwenye tako la bahari, mengine inaonekana kama visiwa, mengine iko chini ya uso wa bahari.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Angalia Historia ya maeneo ya Pasifiki na Historia ya Australia

Mara nyingi kanda nne zimetofautishwa:

Maeneo yanayotajwa kwa "Melanesia" na "Australasia" huingiliana.

Nchi na Maeneo ya Australia na Visiwa vya Pasifiki

[hariri | hariri chanzo]

(Nchi huru zaonekana kwa mwandiko mzito, maeneo yaliyo chini ya nchi nyingine kwa mwandiko wa kawaida)

Jina la eneo,
pamoja na bendera[1]
Eneo
(km²)
Wakazi
(kadiro mnamo
1 Julai 2002)
Msongamano
(watu kwenye km²)
Mji mkuu
Australasia (Australia na New Zealand)
Australia
7,686,850 20,697,241 2.5 Canberra
Kisiwa cha Krismasi (Australia)[2]
135 474 3.5 The Settlement
Visiwa vya Cocos (Keeling) (Australia)[2]
14 632 45.1 West Island
New Zealand[3]
268,680 3,908,037 14.5 Wellington
Kisiwa cha Norfolk (Australia)
35 1,866 53.3 Kingston
Melanesia[4]
Fiji
18,270 856,346 46.9 Suva
Sehemu za Indonesia[5]
499,852 4,211,532 8.4 Jakarta
Kaledonia Mpya (Ufaransa)
19,060 207,858 10.9 Nouméa
Papua Guinea Mpya[6]
462,840 5,172,033 11.2 Port Moresby
Visiwa vya Solomon
28,450 494,786 17.4 Honiara
Vanuatu
12,200 196,178 16.1 Port Vila
Mikronesia
Shirikisho la Mikronesia
702 135,869 193.5 Palikir
Kiribati
811 96,335 118.8 Teinainano
Visiwa vya Marshall
181 73,630 406.8 Majuro
Nauru
21 12,329 587.1 Yaren
Visiwa vya Mariana ya Kaskazini Marekani
477 77,311 162.1 Saipan
Guam (Marekani)
549 160,796 292.9 Hagåtña
Palau
458 19,409 42.4 Melekeok[7]
Polynesia[8]
Samoa ya Marekani (Marekani)
199 68,688 345.2 Fagatogo, Utulei[9]
Visiwa vya Cook (New Zealand)
240 20,811 86.7 Avarua
Polynesia ya Kifaransa (Ufaransa)
4,167 257,847 61.9 Papeete
Hawaii (Marekani)
29,311 1,211,537 42.75 Honolulu
Niue (New Zealand)
260 2,134 8.2 Alofi
Kisiwa cha Pasaka (Chile)
163,6 3,791 23,17 Hanga Roa
Visiwa vya Pitcairn (Uingereza)
5 47 10 Adamstown
Samoa
2,944 178,631 60.7 Apia
Tokelau (New Zealand)
10 1,431 143.1 [10]
Tonga
748 106,137 141.9 Nuku'alofa
Tuvalu
26 11,146 428.7 Vaiaku
Wallis na Futuna (Ufaransa)
274 15,585 56.9 Mata-Utu
Total 9,008,458 35,834,670 4.0
  1. Maeneo hutajwa kufuatana na mpangilio wa Umoja wa Mataifa. Maeneo kadhaa huhesabiwa ama kama nchi za kimabara au sehemu za Asia au Amerika Kaskazini.
  2. 2.0 2.1 Kisiwa cha Krismasi na Visiwa vya Cocos (Keeling) ni maeneo ya Australia katika Bahari Hindi kusini ya Indonesia hivyo hutazamia kuwa sehemu za Asia ya Kusini-Magharibi.
  3. New Zealand mara nyingi huhesabiwa ndani ya Polynesia kuliko Australasia.
  4. Bila Timor ya Mashariki na sehemu za Indonesia ambazo ni visiwa vya Asia lakini huhesabiwa mara nyingi kati ya visiwa vya Pasifiki.
  5. <-- Indonesia kwa jumla ni sehemu ya Asia ya Kusini-Mashariki; sehemu za Guinea Mpya (Irian Jaya) na Visiwa vya Maluku .huhesabiwa humo
  6. [[Papua Guinea Mpya huhesabiwa upande wa Australia lakini pia kwa Melanesia.
  7. Tar 7 Oktoba 2006 serikali ilihamia Melekeok iliyoko takriban kilomita 20 kaskazini ya Koror.
  8. Bila Hawaii ambalo ni jimbo la Marekani. Inahesabiwa mara nyingi kati ya eneo la Amerika ya Kaskazini ingawa ni funguvisiwa ndani ya Pasifiki.
  9. Fagatogo ni makao ya unge na mahakama ya Samoa ya Marekani; Utulei ni makao ya serikali.
  10. Tokelau ni eneo la New Zealand na haina makao makuu kwa jumla kila kisiwa kina chake.
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.