Tasmania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tasmanian Devil,alama ya mnyama wa serikali ya Tasmania
Coat of arms of Tasmania.svg
Flag of Tasmania.svg
Tasmania katika Australia
Bandari ya Hobart

Tasmania ni kisiwa kikubwa upande wa kusini wa Australia bara ni jimbo la Australia lenye eno la 90,758 km². Mji mkuu pia mji mkubwa kisiwani ni Hobart.

Wenyeji asilia[hariri | hariri chanzo]

Wataalamu huamini ya kwamba Tasmania ilikuwa sehemu ya bara la Australia hadi miaka 12,000 iliyopita. Wakati ule watu wameshafika kisiwani lakini kutokea kwa mlango wa bahari kuliwatenga na wenyeji wa Australia. Hivyo walikosa mawasiliano na watu wengine wakaendelea na teknolojia isiyoendelea. Wakati wa kufika kwa Wazungu katika karne ya 17 wenyeji walikuwa na vifaa vichache vya ubao na mawe tu lakini hawakuwa na pinde na mishale, hawakuvua kwa nyavu, hawakujua mashua wala kufuga wanyama au kulima.

Historia ya kikoloni[hariri | hariri chanzo]

Tasmania ilifikiwa na Mholanzi Abel Tasman mwaka 1642 na kupewa jina la "Van-Diemens-Land". Tangu 1803 Uingereza ilivamia kisiwa na kuitumia kama gereza kwa wafungwa kutoka Uingereza au Australia. Walowezi na wafugaji wa kondoo walikuja pia.

Wenyeji asilia waliuawa kwa wingi hadi kupotea kabisa. Leo kuna tu wajukuu wa wanawake wenyeji waliokamatwa na Wazungu na kuzaa nao.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Leo hii kuna takriban watu nusu milioni kisiwani.

 
Majimbo na maeneo ya Australia
Bandera ya Australia
Australia Kusini | Australia ya Magharibi | Australian Capital Territory | New South Wales | Northern Territory | Queensland | Tasmania | Victoria
Australia stub.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Australia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tasmania kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.