Melekeok
Mandhari
Melekeok ni mji mkuu wa nchi ya visiwani ya Palau katika Pasifiki pia mkoa mojawapo wa nchi. Iko kisiwani Babeldaob ambacho ni kisiwa kikubwa cha Palau.
Eneo la mkoa wote wa mji mkuu ni kilomita za mraba 25 na idadi ya wakazi ni 391 (mwaka 2005). Pamoja na Melekeok kuna vijiji saba mkoani.
- Melekeok
- Ertong
- Ngeburch
- Ngeremecheluch
- Ngermelech
- Ngerubesang
- Ngeruling
Karibu na mji kuna ziwa la Ngardok lenye eneo la maji la hektari 492.
Melekeok imekuwa mji mkuu tangu Oktoba 2006.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Seacology Melekeok State Project Ilihifadhiwa 20 Agosti 2009 kwenye Wayback Machine. Seacology
Makala about a place in Australia na Pasifiki bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |