Babeldaob

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kisiwa cha Babeldaob / Babelthuap kwenye kaskazini ya Palau

Babeldaob (pia Babelthuap) ni kisiwa kikubwa cha nchi ya visiwani ya Palau. Eneo lake ni 331 km² au asilimia 70 ya eneo lote la taifa.

Kisiwani kuna mji mkuu wa Melekeok na tisa kati ya mikoa 16 ya Palau.

Maadam visiwa vingine vya Palau ni tambarare kabisa Babeldoab kuna mlima Ngerchelchuus mwenye kimo cha mita 242.

Kwenye mkoa wa Airai upande wa kusini upo uwanja wa ndege wa kimataifa.