Jimbo Kuu la Mwanza
Jimbo Kuu la Mwanza (kwa Kilatini "Archidioecesis Mvanzaënsis") ni mojawapo kati ya majimbo 34 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Chini yake kuna kanda ya Kanisa yenye majimbo yafuatayo: Bukoba, Bunda, Geita, Kayanga, Musoma, Rulenge-Ngara na Shinyanga.
Kanisa Kuu liko jijini Mwanza, na linaitwa la Epifania.
Askofu mkuu wake Yuda Thaddeus Ruwa'ichi, O.F.M.Cap. alihamishiwa Dar es Salaam (2018).
Historia
[hariri | hariri chanzo]- 1880: Kuanzishwa kwa Apostolic Vicariate ya Nyanza kutokana na Apostolic Vicariate ya Central Africa huko Sudan
- 1883: Jina kubadilishwa na kuwa Victoria-Nyanza
- 10 Aprili 1929: Jina kubadilishwa tena na kuwa Mwanza
- 25 Machi 1953: Kupandishwa cheo kuwa dayosisi
- 18 Novemba 1987: Kufanywa jimbo kuu la Mwanza
Uongozi
[hariri | hariri chanzo]- Maaskofu wakuu
- Yuda Thaddeus Ruwa'ichi O.F.M. Cap. (tangu 10 Novemba 2010)
- Anthony Mayala (tangu 18 Novemba 1987 hadi kifo chake 20 Agosti 2009)
- Maaskofu
- Vicars Apostolic
- Joseph Blomjous, M. Afr. (25 Juni 1950 – 25 Machi 1953)
- Antoon Oomen, M. Afr. (18 Machi 1929 – 1950)
Takwimu
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kumegwa (2010) ili kuanzisha jimbo la Bunda, eneo la jimbo lina kilometa mraba 40,000 hivi, ambapo kati ya wakazi 2,600,000, Wakatoliki ni 627,000 (sawa na 24.1%) na wanaunda parokia 27.
Mapadri ni 73, ambao kati yao 41 ni wanajimbo na 32 watawa. Hivyo kwa wastani kila mmojawao anahudumia waamini 8,589.
Jimbo lina pia mabruda 8 na masista 209.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Giga-Catholic Information
- [1]
- [2] Archived 14 Julai 2014 at the Wayback Machine. katika Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
- Hati Litteris Apostolicis Nostris, AAS 21 (1929), uk. 623
- Hati Quemadmodum ad Nos, AAS 45 (1953), uk. 705
- Hati Universae Ecclesiae
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Kuu la Mwanza kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |