Jimbo Katoliki la Bunda
Mandhari
Jimbo Katoliki la Bunda (kwa Kilatini "Dioecesis Bundana") ni mojawapo kati ya majimbo 34 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Eneo lake ni la kilometa mraba 5,330 (wilaya ya Bunda, wilaya ya Ukerewe na parokia mbili katika wilaya ya Bunda vijijini) na lina wakazi 1,023,397 (2004), ambao kati yao Wakatoliki ni 335,000 (32.7 %). Parokia ziko 13.
Kikanisa linahusiana na Jimbo Kuu la Mwanza.
Askofu wake ana makao Bunda mjini. Kanisa kuu limejengwa kwa heshima ya Mtume Paulo.
Anasaidiwa na mapadri 22, ambao kati yao 20 ni wanajimbo na 2 ni watawa. Kwa wastani kila mmojawao anahudumia waamini 15,227. Pia kuna masista 20.
Historia
[hariri | hariri chanzo]- 27 Novemba 2010: Kuanzishwa kwa jimbo jipya kutokana na jimbo kuu la Mwanza na jimbo la Musoma.
Uongozi
[hariri | hariri chanzo]- Askofu Simon Chibuga Masondole kuanzia tarehe 4 Julai 2021
- Askofu Renatus Leonard Nkwande (kuanzia tarehe 27 Novemba 2010 hadi 11 Februari 2019, alipoteuliwa kuwa Askofu mkuu wa Mwanza)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Bunda kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |