Nenda kwa yaliyomo

Kanda ya Kanisa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kanda ya Kanisa (au metropolitani) ni mpango wa uongozi ndani ya baadhi ya madhehebu ya Ukristo.

Kutokana na mpango huo maaskofu wa eneo fulani wanasimamiwa na askofu mkuu wa kanda anayeitwa "metropoliti".

Mamlaka ya askofu wa jimbo kuu juu ya majimbo ya kandokando (yanayoitwa "sufragani") inategemea ile ya Papa wa Kanisa la Roma juu ya majimbo yote duniani. Ndiye anayemshirikisha askofu mkuu ili ayasimamie kadiri ya Sheria za Kanisa. Anatakiwa kuwa na makao katika mji muhimu upande wa Kanisa.

Pengine Waanglikana wanahesabu kama kanda ya Kanisa (kwa Kiswahili wanaiita "jimbo") nchi ambamo ushirika huo umefikia hatua ya kujitegemea, k.mf. "Jimbo la Tanzania", ambalo lina askofu mkuu mmoja bila ya kutegemea umuhimu wa dayosisi yake.

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kanda ya Kanisa kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.