Bikira Maria wa Loreto
Bikira Maria wa Loreto ni jina mojawapo la Bikira Maria lililotokana na kijiji cha Loreto katika mkoa wa Marche, Italia ya Kati, kilichopata umaarufu kutokana na Basilika lililotembelewa na Wakatoliki wengi tangu karne ya 14[1].
Ndani ya kanisa hilo kubwa iko nyumba ndogo inayosemekana kuwa nyumba ya Bikira Mariamu alipopokea ujumbe wa malaika kuwa atapata mimba (linganisha Luka 1). Kuna vyanzo vya kihistoria vinavyodokeza pale Nazareti kulikuwa na jengo dogo lililoheshimiwa kama "nyumba ya Bikira Mariamu". Katika karne ya 14, wakati wa vita katika Palestina ambako makanisa mjini Nazareti yaliharibiwa, mawe kutoka jengo hilo yalipelekwa kwanza hadi Dalmatia (Kroatia ya leo) na baadaye hadi Loreto. Hali halisi kuna matofali katika jengo hilo ndani ya kanisa ambayo yanaweza kutoka Palestina. Uhamisho huo wa matofali ulitekelezwa na familia moja iliyoitwa Angeli[2].
Katika imani ya wenyeji malaika (kwa Kiitalia: angeli) walihamishia nyumba kutoka Nazareti.
Kumbukumbu yake huadhimishwa tarehe 10 Desemba.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/80900
- ↑ Paolo Berti O.F.M.Cap. "The Holy House of Loreto, in the light of archives and archaeology", www.perfettaletizia.it. iliangaliwa desemba 2020.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Grimaldi, Floriano (1984). La Chiesa di Santa Maria di Loreto nei documenti dei secoli XII - XV (kwa Kiitaliano na Kilatini). Ancona: Stabilimento Tipografico Mierma.
- Grimaldi, Floriano (1993). La historia della Chiesa di Santa Maria de Loreto (kwa Kiitaliano). Loreto: Carilo.
- Hutchison, William Antony (1863). Loreto and Nazareth: Two Lectures, Containing the Results of Personal Investigation of the Two Sanctuaries. London: E. Dillon.
- Leopardi, Monaldo (1841). La Santa Casa di Loreto: discussioni istoriche e critiche (kwa Kiitaliano). Lugano: presso Francesco Veladini e C. uk. 1.
- Vélez, Karin (2018). The Miraculous Flying House of Loreto: Spreading Catholicism in the Early Modern World. Princeton University Press. ISBN 978-0-691-18449-4.
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bikira Maria wa Loreto kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |