Nenda kwa yaliyomo

Macau

(Elekezwa kutoka Makau)
Macau
Mkoa maalum wa utawala wa China
澳門特別行政區 (Kichina)
Região Administrativa Especial de Macau da República Popular da China(Kireno)
Eneo la Macau
Lugha rasmiKichina
· Kireno
  Mtendaji mkuu
Ho Iat Seng
  Kuanzishwa kwa mji
Karne ya 5 BK
  Iliundwa na wenyeji Wachina kutwaliwa na Ureno
1557
  koloni ya Ureno
31 Agosti 1862
  Mkoa mwenye utawala wa pekee wa Jamhuri ya Watu wa China
20 Desemba 1999
Eneo
  Jumlakm2 30.3
Idadi ya watu
  Kadirio la 2015642,900
  Msongamano18,568/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2025
  Jumla $98.64 billioni (ya 139)
PLT (Kawaida)Kadirio la 2025
  Jumla $59.27 bilioni
HDI (2022)0.925 juu sana
SarafuPataca ya Macau
Majira ya saaUTC+8 (MST)
Jina la kikoa.mo
Tanbihi:
1 Mji mkuu ulikuwa "Cidade do Nome de Deus de Macau" au rasi ya Macau yenyewe; makao makuu ya serikali ya koloni yalikaa kwenye tarafa ya Sao Lorenco.
2 Habari kutoka Direcção dos Serviços de Estatística e Censos (ofisi ya takwimu ya Macau )
Makao Makuu ya serikali ya Macau

Macau (Kireno: Macau; Kichina: 澳門; pinyin: Àomén), rasmi Mkoa Maalum wa Utawala wa Macao, ni jiji la pwani na Mkoa Maalum wa Utawala (SAR) lilio kusini mwa Uchina, likiingilia kati ya Delta ya Mto Pearl kutoka Hong Kong. Kwa eneo la kilomita za mraba 32.9 (maili 12.7), ni mojawapo ya maeneo yenye idadi kubwa ya watu kwa kilomita za mraba duniani, na idadi ya watu inakadiriwa kuwa karibu 700,000. Ikiwa imeorodheshwa kuwa ya 184 kwa ukubwa wa eneo, Macau ina msongamano mkubwa wa watu wa takriban 21,000 kwa kila kilomita ya mraba.

Tarehe 23 Oktoba 2018 rais wa China Xi Jinping alizindua rasmi daraja la baharini refu kuliko yote duniani (kilometa 55) linalounganisha Hong Kong, Macau na China bara (mji wa Zhuhai).

Koloni la Ureno

[hariri | hariri chanzo]

Macau ilikuwa kituo cha Ureno tangu karne ya 16 na Wareno wakaikodi tangu mwaka 1670.

Macau kama koloni ilithibitishwa katika Mkataba wa Beijing wa mwaka 1887 kati ya China na Ureno.

Macau kama eneo la pekee la China

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1999 ilirudishwa mikononi mwa serikali ya China lakini kwa hali ya pekee inayofanana na ile ya eneo la jirani la Hong Kong.

Hivyo Macau inaendendelea kuratibu yenyewe mambo yake kwa ndani, lakini madaraka kuhusu usalama, jeshi na siasa ya nje yako Beijing.

Wakazi wengi (88.4%) ni Wachina asilia, 1.8% ni Wareno. Kwa kuwa uzazi ni mdogo sana, kuna wahamiaji wengi, hasa Wafilipino (4.6%) na Wavietnam (2.4%).

Lugha rasmi ni Kichina na Kireno. Katika matumizi ya kawaida, Kichina cha Canton kinaongoza (87.5%), na Kiingereza kina waongeaji wengi (2.8%) kuliko Kireno (0.7%).

Upande wa dini, 58.9% wanafuata dini za jadi za Kichina (mchanganyiko wa Ukonfusio na Utao), 17.3% ni Wabuddha au Watao, 7.2% ni Wakristo. 15.4% hawana dini yoyote.

Uchumi wa Macau hutegemea utalii na hasa michezo ya kamari. Kuna pia viwanda vya nguo.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Taarifa za jumla
Utalii
Malezi
Michezo

22°10′N 113°33′E / 22.167°N 113.550°E / 22.167; 113.550

Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Macau kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.