Leopold Sedar Senghor
Léopold Sédar Senghor | |
Rais wa kwanza wa Senegal
| |
Muda wa Utawala 6 Septemba 1960 – 31 Disemba 1980 | |
Waziri Mkuu | Abdou Diouf |
---|---|
mtangulizi | Office created |
aliyemfuata | Abdou Diouf |
tarehe ya kuzaliwa | Joal, Afrika ya Magharibi ya Kifaransa (leo Senegal) | 9 Oktoba 1906
tarehe ya kufa | 20 Desemba 2001 (umri 95) Verson, Ufaransa |
chama | Chama cha Kisoshalisti cha Senegal |
ndoa | Ginette Éboué (1946-1956) Colette Hubert Senghor (m. 1957–2001);hadi kifo |
mhitimu wa | Chuo Kikuu cha Paris |
dini | Kanisa Katoliki |
signature |
Léopold Sédar Senghor (9 Oktoba 1906 – 20 Desemba 2001) alikuwa mshairi, mwanasiasa na hatimaye rais wa kwanza wa Senegal kati ya miaka 1960 na 1980.
Senghor alikuwa Mwafrika wa kwanza aliyechaguliwa kuwa mwanachama wa Académie française. Kabla ya uhuru wa nchi yake aliunda chama cha Umoja wa Kidemokrasia wa Senegal (kwa Kifaransa: Bloc démocratique sénégalais; kwa Kiingereza: Senegalese Democratic Bloc). Wengi wanamhesabu kati ya wataalamu Waafrika muhimu zaidi katika karne ya 20.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Senghor alizaliwa katika kijiji cha Joal kilichowahi kuwa kati ya vituo vya kwanza vya wafanyabiashara kutoka Ulaya na pia kitovu cha misheni Za Kanisa Katoliki kwenye pwani ya Senegal. Baba yake alikuwa mfanyabiashara mzalendo, mama yake mke wa tatu wa baba na Muislamu.
Alipokuwa na umri wa miaka 8 alianza kusoma shule ya mapadre akaendelea kwenye seminari ya mapadri wa Roho Mtakatifu na baada ya kushauriwa asiendelee na masomo ya upadre alisoma shule ya kawaida.
Alimaliza vema hasa kwa masomo ya Kifaransa na Kilatini akapewa nafasi ya kusoma chuo Ufaransa [1].
Mwaka 1928 Senghor alikwenda Ufaransa aliposoma lugha [2] na baadaye sarufi ya Kifaransa kwenye Chuo Kikuu cha Paris. Baada ya masomo alipewa nafasi ya kufundisha kwenye vyuo vya Tours na Paris. Mwaka 1932 alipata uraia wa Ufaransa.
Tangu siku zake masomoni alikuwa na urafiki na Aime Cesaire na pamoja naye alibuni hoja ya "negritude" walipotetea kuwepo kwa utamaduni wa "Watu Weusi" kama utamaduni wa pekee na muhimu, tofauti na utamaduni wa Kizungu.
Mwaka 1945, baada ya vita vikuu vya pili na ushindi wa Ufaransa, alijiunga na chama cha kisoshalisti akachaguliwa kuwa mbunge.
Mwaka 1960 alichaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Senegal akaendela kushika nafasi hiyo hadi mwaka 1980 alipong'atuka kwa hiari.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Bryan Ryan. Major 20th-Century Writers: a selection of sketches from contemporary authors, Volume 4, Gale Research, 1991. ISBN 0-8103-7915-5, ISBN 978-0-8103-7915-2
- ↑ Janet G. Vaillant. Black, French, and African: a life of Léopold Sédar Senghor, Harvard University Press, 1990. ISBN 0-674-07623-0, ISBN 978-0-674-07623-5
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Leopold Sedar Senghor kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |