Jimbo Kuu la Songea
Jimbo Kuu la Songea (kwa Kilatini Archidioecesis Songeana) ni mojawapo kati ya majimbo makuu 7 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania, likiongoza majimbo ya kusini, yakiwemo Mbinga, Tunduru-Masasi, Mtwara, Lindi na Njombe.
Makao makuu ni mjini Songea, ambapo pana Kanisa kuu la mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba.
Takwimu (mwaka 2004)
[hariri | hariri chanzo]Jimbo lenyewe la Songea lina waamini 223.111 (46.9%) kati ya wakazi 476.161 wa eneo lote la kilometa mraba 38,600.
Mapadri ni 105, ambao kati yao 62 ni wanajimbo na 43 watawa. Hivyo kwa wastani kila mmojawao anahudumia Wakatoliki 2,124 katika parokia 27.
Pia jimboni wanaishi mabruda 227 na masista 458.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Baada ya hatua mbalimbali ya uinjilishaji chini ya wamonaki Wabenedikto, tarehe 6 Februari 1969 jimbo liliundwa rasmi, halafu tarehe 18 Novemba 1987 lilifanywa jimbo kuu kwa hati Christi Domini ya Papa Yohane Paulo II.
Maaskofu
[hariri | hariri chanzo]- Willibrord Lay, O.S.B. † (1913 - 1922)
- Gallus (Bernhard) Steiger, O.S.B. † (22 Februari 1922 - 6 Desemba 1952 kujiuzulu)
- Eberhard (Hermann) Spiess, O.S.B. † (23 Septemba 1953 - 6 Februari 1969 kujiuzulu)
- James Joseph Komba † (6 Februari 1969 - 1 Februari 1992)
- Norbert Wendelin Mtega (6 Julai 1992 - 15 Mei 2013 kujiuzulu)
- Damian Dallu (14 Machi 2014 - )
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- [www.catholic-hierarchy.org ukurasa [1]
- (Kiingereza) [2] Archived 18 Julai 2007 at the Wayback Machine. katika tovuti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
- Hati Non sine magna, AAS 20 (1928),uk. 97
- Hati Ex orientali parte, AAS 24 (1932),uk. 262
- Hati Christi Domini
- (Kiingereza) Scheda dell'arcidiocesi su www.gcatholic.com
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Kuu la Songea kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |