Jimbo Katoliki la Lindi
Mandhari
Jimbo Katoliki la Lindi (kwa Kilatini "Dioecesis Lindiensis") ni jimbo la Kanisa Katoliki lenye makao makuu mjini Lindi katika kanda ya Songea upande wa kusini nchi Tanzania.
Kama majimbo yote 34 ya nchi hiyo, linafuata mapokeo ya Roma.
Eneo la jimbo lina kilometa mraba 56,060, ambapo wanaishi wakazi 791.306 (2004), wengi wao wakiwa Waislamu. Kati yao Wakatoliki ni 128.438, sawa na asilimia 16.2, nao wanaunda parokia 26.
Askofu wa jimbo ni Bruno Pius Ngonyani. Mapadri ni 51, ambao kati yao 48 ni wanajimbo na 3 watawa. Kwa wastani kila padri anahudumia waamini 2,518.
Mlolongo wa Maaskofu
[hariri | hariri chanzo]- Arnold Ralph Cotey, S.D.S. † (5 Agosti 1963 - 11 Novemba 1983 kujiuzulu)
- Polycarp Pengo (11 Novemba 1983 - 17 Oktoba 1986 kuhamishiwa Jimbo Katoliki la Tunduru-Masasi)
- Maurus Libaba † (17 Oktoba 1986 - 3 Machi 1988 kufariki dunia)
- Bruno Pius Ngonyani, tangu 6 Oktoba 1990
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- www.catholic-hierarchy.org katika ukurasa [1]
- (Kiingereza) [2] katika www.gcatholic.com
- (Kiingereza) [3] Archived 14 Julai 2014 at the Wayback Machine. Habari za jimbo katika tovuti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
- Hati Quotiens datur kwa Kilatini
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Lindi kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |