Jimbo Katoliki la Mtwara
Mandhari
Jimbo Katoliki la Mtwara (kwa Kilatini "Dioecesis Mtuarana") ni jimbo la Kanisa Katoliki lenye makao makuu mjini Mtwara katika kanda ya Songea upande wa kusini nchi Tanzania.
Kama majimbo yote 34 ya nchi hiyo, linafuata mapokeo ya Roma.
Eneo la jimbo lina kilometa mraba 7,780, ambapo wanaishi wakazi 859,000 (2013), wengi wao wakiwa Waislamu. Kati yao Wakatoliki ni 73,700, sawa na asilimia 8.6, nao wanaunda parokia 18.
Askofu wa jimbo ni Titus Joseph Mdoe. Mapadri ni 42, ambao kati yao 23 ni wanajimbo na 19 watawa. Kwa wastani kila padri anahudumia waamini 1.754.
Historia
[hariri | hariri chanzo]- 22 Desemba 1931: Kuundwa kwa Abasia nullius ya Ndanda kutokana na Jimbo Katoliki la Lindi
- 18 Desemba 1972: Kuundwa kama jimbo kamili.
Mlolongo wa Maaskofu
[hariri | hariri chanzo]- Jimbo la Mtwara
- Askofu Titus Joseph Mdoe
- Askofu Gabriel Mmole (tangu 12 Machi 1988 - 15 Oktoba 2015)
- Askofu Maurus Libaba (18 Desemba 1972 – 17 Oktoba 1986)
- Abasia nullius ya Ndanda
- Askofu Anthony Victor Hälg, O.S.B. (15 Desemba 1949 – 1972)
- Askofu Joachim Ammann, O.S.B. (29 Mei 1932 – 15 Desemba 1948)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Mtwara kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |