Nenda kwa yaliyomo

Uislamu nchini Botswana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uislamu kwa nchi

Uislamu nchini Botswana ni dini ya tatu kwa ukubwa nchini Botswana, ikifuata Ukristo na dini za jadi. Waislamu wana asilimia chini ya 1 ya idadi ya wakazi wote wa nchi hiyo.

Uislamu uliingia nchini humo kupitia wahamiaji kutoka Kusini mwa Asia, ambao walilowea katika eneo hilo wakati wa Ukoloni wa Kiingereza.

Uhusiano baina ya dini tofauti unabaki kuwa wa amani na utulivu, licha ya kuibuka kwa migogoro ya kidini katika maeneo mengine ya bara la Afrika.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]