Nenda kwa yaliyomo

Uislamu barani Asia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uislamu kwa nchi

Uislamu ulianza barani Asia katika karne ya 7 wakati wa zama za uhai wa Mtume Muhammad. Idadi kubwa ya wafuasi wa dini ya Kiislamu wameishi huko Asia na hasa mjini Magharibi mwa Asia na Kusini tangu kuanza kwa historia ya Uislamu.

Uislamu unasemekana kufika mjini Manipur (Kaskazini mashariki mwa India) mwaka 615 kupitia mjini Chittagong ambayo ni sehemu ya pwani ya Bangladesh ya leo katika zama za biashara ya njia ya hariri (vyote, nchi kavu na baharini) wakati Sa'ad ibn abi Waqqas (594-674) na wengine walioitwa Uwais al-Qarni (594-657), Khunais ibn Hudhaifa, Saeed ibn Zaid, Wahb Abu Kabcha, Jahsh na Jafar ibn Abu Talib - walitoa dawah kule.

Hali ya sasa

[hariri | hariri chanzo]

Uislamu kwa sasa ndiyo dini kubwa barani Asia ikiwa na asilimia 25% ikifuatiwa na Uhindu[1] Idadi kamili ya Waislamu barani Asia mnamo mwaka wa 2010 ilikuwa kwenye bilioni 1.1 (sawa na asilimia 25 ya wakazi wote wa Asia).

Asia ni nyumbani pa makundi makubwa ya Waislamu, Mashariki ya Kati ikiwa na (Magharibi/Kusinimagharibi mwa Asia), Asia ya Kati, Asia Kusini na Kusinimashariki mwa Asia ikiwa kama dini muhimu sana.

Asilimia 62 ya Waislamu duniani kote wanaishi Asia, ikiwa ni pamoja na Indonesia, Pakistan, India na Bangladesh, nchi zenye idadi kubwa ya Waislamu duniani.

Uenezi wa Uislamu nje ya Ulimwengu wa Kiarabu kuingia katika sehemu nyingine za bara ulienezwa hasa kwa safari za kibiashara zilizounganishwa kutoka Mashariki ya Kati hadi huko China.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. [1] Archived 18 Januari 2013 at the Wayback Machine. accessed April 3, 2012.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]

Kigezo:Asia in topic