Uislamu barani Ulaya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uislamu barani Ulaya
kwa kulinganisha idadi kwa asilimia[1]
     < 1%
     1–2%
     2–4%
     4–5%
     5–10%
     10–20%
     20–30% Cyprus
     30–40% Jamhuri ya Macedonia
     40–50% Bosnia–Herzegovina
     80–90% Albania
     90–95% Kosovo
     95–100%

Uislamu ulianza kushika hatamu katika bara la Ulaya mnamo mwaka wa 711 kutokana na ushindi wa Umayyad wa Hispania. Waliendelea hadi huko Ufaransa lakini mwaka 732, walishindwa na Wafranki katika Mapigano ya Tours.

Kadiri karne zilivyoenda Waumayyad walikuwa wanakimbizwa kusini polepole na mnamo 1492 Wamoor wa Imarati ya Granada walisalimu amri kwa Watawala Wakuu wa Kikatoliki - Ferdinando V na Isabella. Raia wa Kiislamu walifukuzwa nchini Hispania na ulipofika mwaka 1614 hakuna aliyesalia.[2]

Uislamu uliingia Mashariki na Kusini-Mashariki mwa Ulaya katika sehemu ambazo sasa ni Urusi na Bulgaria katika karne ya 13. Dola la Ottoman lilienea huko na kuchukua nafasi za Ufalme wa Byzanti katika karne ya 14 na 15.

Kadiri karne zilivyoenda, Milki ya Osmani nayo ilipoteza karibia maeneo yake yote ya Ulaya, hadi hapo ilipoanguka rasmi mnamo 1922. Hata hivyo, sehemu za Balkans (kama vile Albania, Kosovo, na Bosnia) ziliendelea kuwa na idadi kubwa ya Waislamu.

Mwisho mwa karne ya 20 na mwanzoni mwa karne ya 21 idadi kubwa ya Waislamu walihamia barani Ulaya. Kunako mwaka wa 2010 ilikadiriwa kuwa Waislamu wanaoishi Ulaya wamefikia milioni 44.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Uislamu kwa nchi

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Soma zaidi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]