Nenda kwa yaliyomo

True Jesus Church

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Sahihi Yesu Kanisa)
True Jesus Church katika kituo cha mafunzo cha bustani ya oliveBandari ya Dickson, Malaysia.


True Jesus Church ni kanisa la kujitegemea la Ukristo wa Kiprotestanti lililo na asili huko Beijing, Uchina, mwaka 1917.

Kanisa hilo linaamini teolojia ya "Mungu Mmoja wa Kweli".

Mwenyekiti wa sasa wa TJC International Assembly aliyechaguliwa ni mhubiri Yong-Ji Lin.

Kwa sasa, kuna wanachama takriban milioni 1.5 hadi 3 katika nchi sitini na tano za mabara sita.

Idadi kubwa wako ndani ya Uchina ambako si rahisi kuhakikisha idadi kamili kwa sababu TSC ni kati ya makanisa na vikundi vya Kikristo vilivyopigwa marufuku na serikali ya nchi hiyo.

Tovuti za TJC katika nchi mbalimbali zinataja Wakristo 70,000 hadi 80,000 katika "nchi huru", wengi wao wakiwa na asili ya Kichina.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kanisa lilianzishwa wakati wa kustawishwa kwa harakati za Kipentekoste nchini Uchina mwanzo wa karne ya 20. Harakati hizi zilianzia Marekani wakati wa mkutano wa kwanza wa Kipentekoste katika Azusa Street Revival huko Los Angeles iliyoongozwa na William J. Seymour miaka [1906]]-1908.

Toka huko tapo hilo lilienea hadi Uchina.

Kulikuwepo moja ya nyumba tatu za Kichina zilizotengenezwa kabla ya Chama cha Kikomunisti cha Uchina kuchukua mamlaka mwaka 1949.

Kanisa lina lengo la kuhubiri injili kwa kila nchi kabla ya kurejea kwa Yesu Kristo.

Tangu mwaka 2002 lilianza kuwasiliana na kikundi cha kikristo huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kilichojiunga nalo mnamo mwaka 2004.

Mafundisho

[hariri | hariri chanzo]

Wanajieleza kwamba Yesu Kristo alianzisha Kanisa moja la kimitume lililopeleka Injili katika nchi mbalimbali. Lakini Kanisa hilo likavurugika na kupatwa na imani potovu na uzushi hadi mwaka 1917 Mungu alipoamua kulifufua kwa nguvu ya Roho Mtakatifu na ndio mwanzo wa TJC.

Kati ya imani nyingine za pekee ni hizi zifuatazo:

  • Atakayebatizwa lazima akubali TJC ni Mwili wa Kristo.
  • Wakanusha mafundisho ya Utatu wa Mungu wakisema "Yesu yu Mungu wa kweli".
  • Wanakataza ibada za Jumapili wakidai siku ya Jumamosi ndiyo siku takatifu ya Sabato iliyoamriwa na Mungu.
  • Hawasheherekei sikukuu za Krismasi na Pasaka kwa sababu wanaamini zina asili za kipagani na ni mifano ya imani ya Kikristo ya asili kuingiliwa na uzushi.
  • Wanaangalia desturi ya kuosha miguu kama sakramenti iliyoamriwa na Yesu.

Mafundisho mengine yanafanana na yale ya Wapentekoste, kama vile kusema kwa lugha za roho au kubatizwa kwa jina la Yesu kwa kuzamishwa chini ya maji, tena maji ya kutiririka.

Imani kuu kumi za kanisa ni:

[hariri | hariri chanzo]
  1. Roho Mtakatifu: "kupatwa na Roho Mtakatifu ambayo huthibitishwa na uwezo wa kuongea pepo, ni hakikisho yetu ya kurithi ufalme mbinguni."
  2. Ubatizo: "Kubatizwa kwa maji ni sakramenti ya kutubu dhambi na kuzaliwa tena. Ubatizo unafaa kufanywa kwenye maji ya kawaida kama vile kwenye mto, kisima au ziwa. Mbatizaji, ambaye pia amebatizwa vilevile na kwa Roho Mtakatifu, hutimiliza ubatizaji kwa jina la Mwana Yesu Kristu. Kichwa cha Mbatizwaji hutumbUkizwa kwenya maji kukamilisha ubatizo."
  3. Kutakaswa: "Sakramenti ya kunawa miguu huwezesha binafsi kuwa na shirika na Bwana Yesu. Pia hutukumbusha mara kwa mara ni lazima tuwe na upendo, utakatifu, unyeyekevu, msamaha na utumishi. Yeyote aliyepata ubatizo wa maji ni lazima aoshwe miguu kwa jina la Yesu Kristo. Kunawishwa miguu yaweza kufanywa inapohitajika."
  4. Komunio Takatifu: "Komunio Takatifu ni sakramenti ya kusheherekea kifo cha Mola Yesu Kristu. Inatueneza kupata mwili na damu ya mwokozi wetu na kuwa na umoja naye ili tuweze kupata uzima wa milele na kufufuliwa siku ya mwisho. Sakramenti hii ina haja ya kufanywa kila iwezekanapo. Katika sakramenti hii hutumiwa mkate na divai."
  5. Sabato: "Siku ya sabato, ambayo ni siku ya saba kwenye wiki (Jumamosi), ni siku takatifu, iliyobarikiwa na kusahihishwa na Mungu Baba. Siku hii hubudiwa kwa ajili ya ukumbusho wa maumbo na pia ukombozi na Mungu Baba, na tarajio la pumziko la milele daima kwenye maisha yatakayokuja."
  6. Yesu Kristo: "Yesu Kristo, Neno aliyefanyika mwili, akafa msalabani kwa msamaha wa wenye dhambi, akafufuka siku ya tatu akapaa juu mbinguni. Yeye ndiye mwokozi wa binadamu, Muumba wa mbingu na nchi na ndiye Mungu wa kweli."
  7. Biblia Takatifu (Maandiko Matakatifu): "Biblia Takatifu, ina Agano la Kale na Agano Jipya ambayo imewezeshwa na Mungu na yenye Maandiko Matakatifu ya kweli kwa maisha ya Mkristo."
  8. Wokovu: "Wokovu unatolewa kwa neema ya Mungu kupitia imani. Waaminio lazima wamwamini Roho Mtakatifu ili kupata utakatifu, kwa kumheshimu Mungu, na kwa upendo wa watu"
  9. Kanisa: "Kanisa, lililetwa na Bwana Yesu Kristo, kupitia Roho Mtakatifu kipindi cha 'nyakati za mwisho', ni kanisa la kweli lililorejeshwa nyakati za ki'Apostoliki."
  10. Hukumu ya mwisho: "Kuja kwa Yesu kwa mara ya pili itakuwa siku ya mwisho wakati akishuka kutoka mbinguni kuhukumu: walio na haki watapokea uzima wa milele wasio na haki watahukumiwa milele"

Hoja ya msingi

[hariri | hariri chanzo]

Ingefaa ueleweke ukweli wa msimamo wa TJC kulingana na Biblia wanapodai kwa miaka mia kadhaa duniani halikuwepo tena Kanisa la kweli, wakati Yesu aliahidi, "Nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari" (Mathayo 28:20). Tena "Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda" (Mathayo 16:18).

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu True Jesus Church kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.