10 Oktoba
Mandhari
(Elekezwa kutoka Oktoba 10)
Sep - Oktoba - Nov | ||||||
1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 |
8 | 9 | 10 | 11 | 12 | 13 | 14 |
15 | 16 | 17 | 18 | 19 | 20 | 21 |
22 | 23 | 24 | 25 | 26 | 27 | 28 |
29 | 30 | 31 | ||||
Kalenda ya Gregori |
Tarehe 10 Oktoba ni siku ya 283 ya mwaka (ya 284 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 82.
Matukio
[hariri | hariri chanzo]- 680 - Mapigano ya Karbala (Aashurah): Hussein ibn Ali, mjukuu wa Muhamad, anakatwa kichwa na Waislamu wenzake
- 732 - Mapigano ya Tours na Poitiers (Ufaransa) - uvamizi wa Waarabu katika Ulaya Magharibi unasimamishwa na jeshi la Wafaranki linaloongozwa na Karolo Martell. Jemadari Abdul Rahman Al Ghafiqi anauawa na Waarabu wenzake wanarudi Hispania
- 1868 - Nchi ya Kuba inapata uhuru kutoka Hispania
Waliozaliwa
[hariri | hariri chanzo]- 786 - Saga, mfalme mkuu wa Japani (809-823)
- 1861 - Fridtjof Nansen, mpelelezi na mwanasiasa Mnorwei na mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani mwaka wa 1922
- 1892 - Ivo Andric, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka wa 1961
- 1913 - Claude Simon, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka wa 1985
- 1917 - Thelonious Monk, mwanamuziki wa Marekani
- 1930 - Harold Pinter, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka wa 2005
- 1930 - Yves Chauvin, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 2005
- 1936 - Gerhard Ertl, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 2007
- 1948 - Benedict Kiroya Losurutia, mwanasiasa wa Tanzania
- 1958 - Tanya Tucker, mwimbaji wa Marekani
- 1964 - Quinton Flynn, mwigizaji filamu kutoka Marekani
- 1967 - Gavin Newsom, mfanyabiashara na mwanasiasa wa Marekani
- 1969 - Loren Bouchard, mwigizaji wa filamu kutoka Marekani
- 1979 - Mýa, mwanamuziki wa Marekani
- 1998 - Nash Aguas, mwigizaji filamu kutoka Ufilipino
Waliofariki
[hariri | hariri chanzo]- 644 - Mtakatifu Paulinus wa York, askofu wa kwanza wa York
- 1881 - Mtakatifu Daniele Comboni, askofu Mkatoliki kutoka Italia mmisionari nchini Sudan na Sudan Kusini
- 1985 - Yul Brynner, mwigizaji filamu kutoka Marekani
- 2015 - Richard Heck, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia, mwaka wa 2010
Sikukuu
[hariri | hariri chanzo]Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Pinito wa Knoso, Eulampi na Eulampia, Gereoni na wenzake, Vikta na Maloso, Kasio na Fiorenso, Klaro wa Nantes, Serboni, Tanka, Paulino wa York, Theodeilde, Danieli Fasanella na wenzake, Yohane Twenge, Daniele Comboni n.k.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu 10 Oktoba kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |