Paulinus wa York

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Sanamu ya Mt. Paulinus katika kanisa kuu la Rochester

Paulinus wa York (alifariki 10 Oktoba 644) alikuwa mmisionari kutoka Roma nchini Uingereza aliyefanywa askofu wa kwanza wa York.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Akiwa kati ya wamonaki waliotumwa na Papa Gregori I ili kuinjilisha Waangli na Wasaksoni, Paulinus alifika mwaka 604 katika kundi la pili.

Baada ya kuishi miaka huko Kent, tarehe 21 Julai 625 alipewa daraja takatifu ya uaskofu. Aliposindikiza Æthelburg wa Kent kwenda Northumbria kuolewa na Edwin wa Northumbria, alifaulu kumuongoa Edwin kuingia Ukristo pamoja na raia wake wengi. Kati yao alikuwepo Hilda wa Whitby. Pia alijenga makanisa kadhaa.

Edwin alipofariki (633), Paulinus na Æthelburg walikimbia Northumbria, wakimuacha nyuma James Shemasi. Huko Kent, Paulinus akawa askofu wa Rochester akapokea paliumu kutoka kwa Papa, ikiwa na maana ya kufanywa askofu mkuu wa York, ingawa hakupata nafasi ya kwenda[1].

Tangu kale Paulinus anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

 1. Lapidge "Ecgbert" Blackwell Encyclopedia of Anglo-Saxon England

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

   . http://www.oxforddnb.com/view/article/21626. Retrieved 6 March 2009.
 • Farmer, David Hugh (2004). Oxford Dictionary of Saints, Fifth, Oxford, UK: Oxford University Press. ISBN 978-0-19-860949-0. 
 • (1996) Handbook of British Chronology, Third revised, Cambridge, UK: Cambridge University Press. ISBN 0-521-56350-X. 
 • Kirby, D. P. (2000). The Earliest English Kings. New York: Routledge. ISBN 0-415-24211-8. 
 • Lapidge, Michael (2001). "Ecgberht". The Blackwell Encyclopaedia of Anglo-Saxon England. Malden, MA: Blackwell Publishing. p. 157. ISBN 978-0-631-22492-1
   .
   .
   .

Marejeo mengine[hariri | hariri chanzo]

 • Mayr-Harting, H. M. R. E. (1967). "Paulinus of York". In G. J. Cuming. Studies in Church History IV: The Province of York. Leiden: Brill. pp. 15–21.
Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Paulinus wa York kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.