Hilda wa Whitby

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Hilda katika kioo cha rangi, kanisa kuu la Gloucester Cathedral.
Maghofu ya Abasia ya Whitby.

Hilda wa Whitby (614 hivi – 17 Novemba 680) alikuwa abesi mwanzilishi[1][2] wa monasteri ya Whitby, iliyofuata desturi za Ukristo wa Kiselti. Ndipo palipofanyika Sinodi ya Whitby[3]iliyokubali kufuata desturi za Kanisa la Roma.

Muhimu katika kuvuta Waangli na Wasaksoni katika Ukristo, alisimamia pia monasteri nyingine kwa hekima yake maarufu.

Habari za Hilda zinategemea hasa kitabu cha historia ya Kanisa kilichoandikwa na Beda Mheshimiwa mwaka 731.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake au siku nyingine.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

  • Sister Hilary OHP; (2003). St. Hilda of Whitby, Order of the Holy Paraclete, St. Hilda's Priory, Sneaton Castle, Whitby YO21 3QN.

Marejeo mengine[hariri | hariri chanzo]

  • Bede (1996) The Ecclesiastical History of the English Church and People, Oxford University Press, World classics series.
  • Bradley, Ian (1999) Celtic Christianity, Edinburgh University Press.
  • Cavill, Paul (1999) Anglo-Saxon Christianity: exploring the earliest roots of Christian spirituality in England, London: Collins, Fount paperback.
  • Hume, Basil (1996) Footprints of the Northern Saints, London: Darton, Longman & Todd.
  • Simpson, Ray (2014) Hilda of Whitby: A spirituality for now, BRF
  • Thurston, H. (1910) St. Hilda.
  • Warin, Anne (1989) Hilda, Lamp Press.
  • Watling, Barbara (2005). "St Hilda of Hartlepool and Whitby" (Article). Catholic Life Magazine. Archived from the original on 2011-07-17. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.