Nenda kwa yaliyomo

Serboni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Serboni katika dirisha la kioo cha rangi.

Serboni (kwa Kilatini: Cerbonius; Afrika Kaskazini, 493 - Elba, Toscana, Italia, 575) alikuwa askofu wa Populonia wakati wa uhamisho mkuu wa Ulaya.

Akiwa padri, alihama Afrika ili kukwepa dhuluma ya Wavandali dhidi ya Wakatoliki, akahamia Italia ya Kati alipopata uaskofu.

Walombardi walipovamia eneo hilo, yeye alihamia katika kisiwa cha Elba alipotoa mifano ya utakatifu na kutenda miujiza mingi.

Gregori Mkuu alimsifu katika Kitabu XI cha Majadiliano.[1]

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 10 Oktoba[2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "San Cerbone, il santo patrono di Massa Marittima". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-07-22. Iliwekwa mnamo 2019-09-13.
  2. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.