Nenda kwa yaliyomo

Paulinus wa York

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Paulino wa York)
Mt. Paolino akimbatiza mfalme Edwin.

Paulinus wa York (alifariki 10 Oktoba 644) alikuwa mmisionari kutoka Roma nchini Uingereza aliyefanywa askofu wa kwanza wa York[1].

Akiwa kati ya wamonaki waliotumwa na Papa Gregori I ili kuinjilisha Waangli na Wasaksoni, Paulinus alifika mwaka 604 katika kundi la pili.

Baada ya kuishi miaka huko Kent, tarehe 21 Julai 625 alipewa daraja takatifu ya uaskofu. Aliposindikiza Æthelburg wa Kent kwenda Northumbria kuolewa na Edwin wa Northumbria, alifaulu kumuongoa Edwin kuingia Ukristo pamoja na raia wake wengi[2]. Kati yao alikuwepo Hilda wa Whitby. Pia alijenga makanisa kadhaa.

Edwin alipofariki (633), Paulinus na Æthelburg walikimbia Northumbria, wakimuacha nyuma James Shemasi. Huko Kent, Paulinus akawa askofu wa Rochester akapokea paliumu kutoka kwa Papa, ikiwa na maana ya kufanywa askofu mkuu wa York, ingawa hakupata nafasi ya kwenda[3].

Tangu kale Paulinus anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/92490
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/92490
  3. Lapidge "Ecgbert" Blackwell Encyclopedia of Anglo-Saxon England
  • Blair, Peter Hunter (1990). The World of Bede (tol. la Reprint of 1970). Cambridge, UK: Cambridge University Press. ISBN 0-521-39819-3.
  • Costambeys, Marios (2004). "Paulinus (St Paulinus) (d. 644)". Oxford Dictionary of National Biography (October 2005 revised ed.). Oxford University Press. doi:10.1093/ref:odnb/21626
     . http://www.oxforddnb.com/view/article/21626. Retrieved 6 March 2009.
      .
      .

Marejeo mengine

[hariri | hariri chanzo]
  • Mayr-Harting, H. M. R. E. (1967). "Paulinus of York". In G. J. Cuming. Studies in Church History IV: The Province of York. Leiden: Brill. pp. 15–21.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.