Hussein ibn Ali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Msikiti wa Kaburi la Imamu Hussein mjini Karbala
Taswira ya Kiajemi inayomwonyesha Hussein katika mapigano ya Karbala

Hussein ibn Ali[1] (ar. حسين بن علي‎ , *11 au 13 Januari 626 BK10 Oktoba 680 BK, au 3 Shaabani 4 BH - 10 Muharram 61 BH) (3 شعبان 4 هـ - 10 محرم 61 هـ ) alikuwa mjukuu wa Mtume Muhammad akitazamiwa kama imamu wa kwanza wa Washia. Alizaliwa mjini Makka, babake alikuwa Ali ibn Abi Talib (khalifa wa nne na mamake Fatimah Zahra binti wa Muhammad. Kakaye alikuwa Hasan ibn Ali imamu wa pili wa Washia.

Hussein ibn Ali ni mtu muhimu sana kati ya Washia wanaomwangalia kama mtu mtakatifu kutokana na uhusiano wake wa karibu na mtume Muhammad na kama kielelezo kwa ushujaa wake katika mapigano ya Karbala. Washia wanamkumbuka na kukumsifu kwa upinzani wake dhidi ya Yazid I aliyekuwa khalifa wa Wamuawiya. Aliuawa katika Mapigano ya Karbala pamoja na wengi wa familia yake kwenye siku ya Ashura. Hivyo anatazamiwa kama mfia dini hasa kati ya Washia na kukumbukwa kwenye sherehe za mwezi Muharram, hasa siku za Tasua na Ashura.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Jina lake linaandikwa pia Husayn, Husain, Hussain au Hossein kwa herufi za Kilatini
  2. Nakash, Yitzhak (1 January 1993). "An Attempt To Trace the Origin of the Rituals of Āshurā¸". Die Welt des Islams. 33 (2): 161–181. doi:10.1163/157006093X00063.