Shaaban (mwezi)
Shaaban (kwa Kiarabu: شعبان, sha‘bān) ni mwezi wa nane katika kalenda ya Kiislamu. Inafuata Rajabu ikifuatwa na Ramadan.
Ilhali ni mwezi kabla ya Ramadani ni pia wakati ambako mwanzo wa saumu unatangazwa.[1]
Nisfu Shaaban
Siku ya 15 ya Shaaban inajulikana kama "usiku wa kumbukumbu" au Laylatul Bara-at [2] lakini adhimisho hilo lina utata.[3]. Kufuatana na hadith Mtume Muhammad alitaja tarehe hiyo kuwa siku maalumu, hivyo kuna Waislamu wanaoamini ya kwamba usiku huo una baraka za pekee. Wengine hukaa usiku huo pamoja wakisoma Korani na kushiriki katika sala za pekee. Wengine wanapinga ibada hizo.[4]
Sikikuu ya Imamu Mahdi
Washia Ithna ashari husheherekea tarehe 15 Shaaban kama sikukuu ya kuzaliwa kwa imamu wao wa 12 na wa mwisho, Muhammad al Mahdi.[5]
Tarehe zake
Ilhali kalenda ya Kiislamu ni kalenda ya mwezi miezi yake huanza wakati wa kutazamwa kwa hilali ya mwezi mpya. Pia kwa sababu mwaka wa mwezi ni mfupi kuliko mwaka wa jua basi tarehe za Shaaban zinapita kwenye majira. Tarehe zake kwa miaka ya karibu ni takriban[6]:
Mwaka baada ya Hijra | Siku yake ya kwanza katika kalenda ya BH / AD) | Siku yake ya mwisho katika kalenda ya BH / AD |
---|---|---|
1437 | 8 Mei 2016 | 5 Juni 2016 |
1438 | 28 Aprili 2017[1] | 26 Mei 2017 |
1439 | 17 Aprili 2018 | 15 Mei 2018 |
1440 | 6 Aprili 2019 | 5 Mei 2019 |
1441 | 25 Machi 2020 | 23 Aprili 2020 |
1442 | 14 Machi 2021 | 12 Aprili 2021 |
Tarehe za Shaaban baina ya 2016 BK na 2021 BK |
Kumbukumbu maalumu
- 01 Shaaban, kuzaliwa kwa Zainab bint Ali
- 03 Shaaban, kuzaliwa kwa Hussein ibn Ali
- 04 Shaaban, kuzaliwa kwa Abbas ibn Ali
- 05 Shaaban, kuzaliwa kwa Ali ibn Hussein
- 07 Shaaban, kuzaliwa kwa Qasim ibn Hasan
- 11 Shaaban, kuzaliwa kwa Ali al-Akbar ibn Husayn
- 11 Shaaban 1293 BH, Abdulhamid II alikuwa sultani wa Milki ya Osmani
- 15 Shaaban, sikukuu ya Laylat al-Bara'at au Nusu Shaaban; kuzaliwa kwa Muhammad al-Mahdi
Tazama pia
Marejeo
- ↑ 1.0 1.1 "Ramadan fasting to start May 27 or May 28". www.aljazeera.com. Iliwekwa mnamo 2017-04-27.
- ↑ G.E. von Grunebaum, Muhammadan Festivals (London: Curzon Press, 1976), pp. 53-54.
- ↑ "Bid'ah of Sha'baan - islamqa.info". islamqa.info.
- ↑ Fadhila za mwezi wa Shaaban na uzushi wa Nisfu Shaaban, tovuti ya islamhouse.com, iliangaliwa Septemba 2018
- ↑ A Dazzling Night in Iran Embellished with Spirituality Archived 26 Mei 2015 at the Wayback Machine., taarifa ya mwaka 2014 kwenye tovuti ya realiran.org, iliangaliwa September 2018
- ↑ Umm al-Qura calendar of Saudi Arabia