Washia Ithna ashari
Washia Ithna ashari (ing. Twelfer Shia, pia Ithnaashari) ni kundi kubwa kati ya Waislamu Washia. Wako wengi huko Iran, Irak na Lebanoni.
Jina
[hariri | hariri chanzo]Jina "Ithnaashari" linatokana na namba 12 katika lugha ya Kiarabu اثنا عشرية ithna ashariyya kwa maana ya kwamba wanahesabu maimamu 12 waliomfuata Mtume Muhammad kama viongozi halali wa umma wa Waislamu, tofauti wa Washia wengine wenye makadirio tofauti kuhusu idadi ya maimamu.
Imani
[hariri | hariri chanzo]Huamini ya kwamba Mungu aliwateua binadamu 14 wasioweza kukosa; hao ni Mtume Muhammad, binti yake Fatima na maimamu 12 ambao ni wajukuu wa Muhammad na wana wao. Imamu wa mwisho na wa 12 ni Muhammad al Mahdi aliyeingia katika hali ya mafichoni akipatikana duniani bila kuonekana. Wanasubiri kurudi kwake atakaposhinda maadui wa Mungu na kutawala Dunia. Katika mafundisho mengi hukubaliana na Wailamu wengine lakini wana mafundisho kadhaa ya pekee.
Maimamu 12 ni wafuatao:
- Ali ibn Abi Talib
- Hassan ibn Ali
- Hussein ibn Ali
- Ali ibn Husayn
- Muhammad al-Baqir
- Jafar as-Sadiq
- Musa al-Kadhim
- Ali ar-Ridha
- Muhammad at-Taqi
- Ali al-Haadi
- Hasan al-Askari
- Muhammad al-Mahdi
Kati ya hao wanaheshimu hasa Ali na mwanawe Hussein aliyeuawa katika mapigano ya Karbala.
Chuo Kikuu cha Al Azhar kiliwatambua kama madhhab halali kwa jina la "madhhab ya Jafar"[1]. Sehemu ya Wasunni hasa wanaofuata mafundisho ya Wahabiyya wanawaangalia kama wazushi wasio Waislamu wa kweli.
Jamii zao
[hariri | hariri chanzo]Takriba asilimia 85% za Washia wote ni Ithnaashari. Wako idadi kubwa ya wananchi katika Iran (90%), Irak (65%), Azerbaijan (85%) na and Bahrain (80%).
Jamii kubwa wako pia Lebanoni (35% za wananchi), Kuwait (35%), Uarabuni wa Saudia (10-15%),[2] Pakistan (20%) na Afghanistan (18%).
Nchini Iran ni dini rasmi ya dola.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Al-Azhar Verdict on the Shi’a, tovuti ya al-islam.org, ilitazamiwa Septemba 2018
- ↑ "International Crisis Group. The Shiite Question in Saudi Arabia, Middle East Report N°45, 19 September 2005" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2008-12-17. Iliwekwa mnamo 2018-09-13.