Ramadan (mwezi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya

Uislamu

Historia ya Uislamu

Imani na ibada zake

Umoja wa Mungu
Nguzo za Kiislamu
ShahadaSwalaSaumu
HijaZaka

Watu muhimu

Muhammad

Abu BakrAli
Ukoo wa Muhammad
Maswahaba wa Muhammad
Mitume na Manabii katika Uislamu

Maandiko na Sheria

Qur'anSunnahHadithi
SheriaKalam
Wasifu wa Muhammad
Sharia

Aina za Uislamu

SunniShi'aKharijite

Tamaduni za Kiislamu

ShuleHistoria
TauhidiFalsafaSayansi
SanaaUjenziMiji
KalendaSikukuu
Wanawake
ViongoziSiasa
UmmaItikadi mpyaSufii

Tazama pia

KamusiKuogopa Uislamu

Ramadan au ramadhani, ramazani (kwa Kiarabu رمضان) ni mwezi wa tisa katika Kalenda ya Kiislamu na mwezi wa kufunga katika Uislamu.

Mwislamu mzima, mwenye afya nzuri, anatakiwa kushiriki katika swaumu ambayo ni ibada ya kufunga chakula na kinywaji mchana kutwa, pamoja na kujizuia kufanya mapenzi toka alfajiri hadi magharibi.

Matendo hayo ya toba yanaendana na kuswali sana na kusoma quran kwa wingi.

Mwisho wa Ramadan ni sikukuu ya Idul Fitri (عيد الفطر - ʿīdu ʾl-fiṭr) ambayo ni sherehe ya furaha na kupongezana. Waislamu hutoa zakat (zakatul-fitri زكاة الفطر) na kusali, baadaye hukutana kwenye karamu.

Katika quran, sura 2 aya 185: Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni wongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.

Kusoma Qurani[hariri | hariri chanzo]

“Mwezi wa Ramadhani ambayo imeteremshwa ndani yake Qur-an hali ya kuwa ni uongofu kwa watu …………" Kwa kuwa katika mwezi huu ndio Qurani iliteremshwa kwa Mtume, inatakiwa kwa muislam kufanya bidii kuisoma angalau juzuu moja kwa siku ili aweze kumaliza msahafu ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Ramadhan.

Kuharakisha kufungua[hariri | hariri chanzo]

Miongoni mwa sunna tukufu zinazotakiwa kwa mfungaji katika mwezi huu kuzikimbilia, ni kuharakisha kufungua baada tu ya kuzama jua, kwani Mtume amesema katika hadithi iliopokewa na Tirmidhy, Ibnu khuzayma na Ibnu Habban: “Hakika nimpendaye zaidi miongoni mwa waja wangu ni anayefanya haraka katika wao kufungua saumu.”

Kusali usiku[hariri | hariri chanzo]

Inatakiwa kwa muislam kuyatumia masiku ya mwezi huu mtukufu katika kumuabudu Allah kwa kusali na kufanya ibada nyengine, kwani ni mwezi wa pekee ambao ndani yake kunapatikana usiku wa cheo (Laylatul Qadr) ambao ibada ya usiku huo inalingana na ibada ya miezi elfu moja, na kwa hekima yake Allah hakutubainishia kuwa ni usiku wa tarehe ngapi. Na hii ni moja miongoni mwa fadhila za kusali katika masiku ya mwezi huu. Vile vile mwenye kusimama kwa ibada katika masiku haya husamehewa makosa yake yote yaliyotangulia, kama alivyosema Bwana Mtume: “Mwenye kusimama usiku wa Ramadhani kwa kufanya ibada hali ya kuwa na imani na kutaraji thawabu anasamehewa yoteyaliotangulia miongoni mwa makosa yake.” (Bukhari na Muslim).

Kula daku[hariri | hariri chanzo]

Kula daku vilevile ni miongoni mwa sunna tukufu zinazodharauliwa na wengi kati ya waislam na fadhila zake ni kubwa kupita kiasi, miongoni mwazo ni kurehemewa na Allah na kutakiwa msamaha na malaika watukufu kama alivyosema Mtume katika hadithi: “Hakika Allah na Malaika wake wanawarehemu wenye kula daku.” (Twabrani, Ibnu Habban).

Vile vile Mtume amesisitiza katika hadithi kwa kusema kuwa: “Hakika daku ni baraka amekupeni Allah, hivyo basi musiiache”. (Annasai)

Kukaa Itikaaf[hariri | hariri chanzo]

Inatakiwa kwa muislam kuujaalia mwezi huu na kuutumia katika kuchuma na kuvuna aina tofauti ya mema ikiwemo Itikaaf, kwani ni miongoni mwa ibada bora sana zinazomkurubisha mja kwa Mola wake hasa awapo katika mwezi huu wa Ramadhani, kwani baadhi ya wanavyuoni wamesema kuwa haisihi ibada hii ya itikaaf pasi na funga. Na yatoshe malipo makubwa yaliotajwa katika hadithi; Mtume amesema: “Mwenye kukaa itikaaf siku kumi katika mwezi wa Ramadhani, basi ni kama aliyehiji na akafanya umra mara mbili mbili." (Bayhaq)

Kutoa sadaka[hariri | hariri chanzo]

Miongoni mwa ibada tukufu alizokuwa akizifanya Mtume ni kutoa sadaka na alilipa umuhimu sana jambo hili hadi wakati wa kuondoka kwake ulimwenguni alipokuwa katika sakaratul mauti kila alipopata fahamu ilikuwa akimuuliza Bibi Aisha iwapo ashazitoa sadaka zile dirhamu nne zilizokuwa nyumbani? Kadhalika kutoa huku kwake kulikuwa kukiongezeka katika Ramadhani.

Kumtaja Allah (Subhaanahu wa Ta’ala)[hariri | hariri chanzo]

Katika mwezi huu wa Ramadhani kadhalika inatakiwa kwa muislam kuwa mengi ya maneno yake yawe katika kumtaja Allah (Subhaanahu wa Ta’ala), kwani ni jambo ambalo linasaidia katika kuusafisha moyo wake na kuiboresha funga yake. Allah ametuamrisha tumtaje kwa wingi katika aya nyingi za Qurani, na hii ndio ibada pekee aliyosema Allah kuwa ifanywe kwa wingi, na miongoni mwa aya hizo; “Enyi Mlioamini mtajeni Allah kwa wingi na mumtakase yeye asubuhi na jioni.” (Al- Ahzaab 41 na 42)

Kadhalika Mtume alifundisha aina tofauti za kumtaja Allah ili tusichoke na jambo hili kwani mwanadamu ni mwepesi wa kuchoka na jambo moja tu. Vile vile akatuonyesha tofauti kubwa iliopo kati ya anayemtaja Allah na asiyefanya hivyo kati hadithi aliposema; “Mfano wa anayemtaja Allah na asiyemtaja ni mfano wa mtu aliyehai na aliyekufa.” (Bukhari).

Haya ni baadhi ya yanayotakiwa kufanywa na muislam, hasa awapo ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, hivyo basi tujihimu katika kuyatekeleza haya tuliyoelezwa na tumuombe Allah atutakabaliye matendo yetu “Amin”.

Kuthibiti mwezi wa Ramadhani[hariri | hariri chanzo]

Mas’ala: 1-Huzingatiwa katika kuthibiti kwa mwezi wa ramadhani na kuwajibika kufunga mwezi wa Ramadhani njia hizi zifuatazo:

1- Mukallaf auone mwezi yeye mwenyewe.

2- Apate yakini au matumaini kutokana na kuenea kwa habari za kuonekana kwa mwezi huo au habari zingine zithibitishazo suala hilo katika nchi yake au sehemu yenye hukumu kama hiyo.

3- Kupita siku thalathini za mwezi wa shaaban.

4-Kutoa ushahidi wanaume wawili waadilifu ya kuwa wameuona (na hapo nyuma tumekwisha elezee maana ya uadilifu) na huzingatiwa kuwa kinacho tolewa ushahidi kiwe ni kimoja, lau mmoja wao atadai ya kuwa ameuona mwezi katika upande fulani, na mwingine akadai ya kuwa ameuona upande mwingine, kwa ushahidi huo mwezi hautathibiti, kama ambavyo huzingatiwa kutokuwepo mpingaji wa ushahidi huo - hata kama kwa kuonyesha kitendo chenye hukumu kama hiyo ya kupinga - kama ikiwa kundi la watu fulani wa nchi hiyo watatoa habari za kuonekana mwezi na wakadai kuwa wameuona mwezi na miongoni mwao kukiwemo waadifu wawili, au wakatoa habari za kuonekana mwezi kundi fulani lakini hawakudai ya kuwa wameuona mwezi isipokuwa waadilifu wawili na wengine hawakuuona na miongoni mwao kukiwa na waadilifu wawili ambao ndio wanao wawakilisha katika kufahamu sehemu pekee iliyo onekana mwezi kwa kuangalia pamoja na anga kuwa safi na kutokuwepo kinacho tarajiwa kuwa ni kizuwizi cha kuuona mwezi, katika hali kama hii ushahidi wa watu wawili waadiofu hauna iitibari yoyote, isipo kuwa ikipatikana yakiini na matumaini kutokana na ushahidi wao.

Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ramadan (mwezi) kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.