Shaaban (mwezi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Shaaban (kwa Kiarabu: شعبان, sha‘bān) ni mwezi wa nane katika kalenda ya Kiislamu. Inafuata Rajabu ikifuatwa na Ramadan.

Ilhali ni mwezi kabla ya Ramadani ni pia wakati ambako mwanzo wa saumu unatangazwa.[1]

Nisfu Shaaban

Siku ya 15 ya Shaaban inajulikana kama "usiku wa kumbukumbu" au Laylatul Bara-at [2] lakini adhimisho hilo lina utata.[3]. Kufuatana na hadith Mtume Muhammad alitaja tarehe hiyo kuwa siku maalumu, hivyo kuna Waislamu wanaoamini ya kwamba usiku huo una baraka za pekee. Wengine hukaa usiku huo pamoja wakisoma Korani na kushiriki katika sala za pekee. Wengine wanapinga ibada hizo.[4]

Sikikuu ya Imamu Mahdi

Washia Ithna ashari husheherekea tarehe 15 Shaaban kama sikukuu ya kuzaliwa kwa imamu wao wa 12 na wa mwisho, Muhammad al Mahdi.[5]

Tarehe zake

Ilhali kalenda ya Kiislamu ni kalenda ya mwezi miezi yake huanza wakati wa kutazamwa kwa hilali ya mwezi mpya. Pia kwa sababu mwaka wa mwezi ni mfupi kuliko mwaka wa jua basi tarehe za Shaaban zinapita kwenye majira. Tarehe zake kwa miaka ya karibu ni takriban[6]:

Mwaka baada ya Hijra Siku yake ya kwanza katika kalenda ya BH / AD) Siku yake ya mwisho katika kalenda ya BH / AD
1437 08 Mei 2016 05 Juni 2016
1438 28 Aprili 2017[1] 26 Mei 2017
1439 17 Aprili 2018 15 Mei 2018
1440 06 Aprili 2019 05 Mei 2019
1441 25 Machi 2020 23 Aprili 2020
1442 14 Machi 2021 12 Aprili 2021
Tarehe za Shaaban baina ya 2016 BK na 2021 BK

Kumbukumbu maalumu

Tazama pia

Marejeo

  1. 1.0 1.1 Ramadan fasting to start May 27 or May 28.
  2. G.E. von Grunebaum, Muhammadan Festivals (London: Curzon Press, 1976), pp. 53-54.
  3. Bid‘ah of Sha‘baan - islamqa.info. islamqa.info.
  4. Fadhila za mwezi wa Shaaban na uzushi wa Nisfu Shaaban, tovuti ya islamhouse.com, iliangaliwa Septemba 2018
  5. A Dazzling Night in Iran Embellished with Spirituality Archived 26 Mei 2015 at the Wayback Machine., taarifa ya mwaka 2014 kwenye tovuti ya realiran.org, iliangaliwa September 2018
  6. Umm al-Qura calendar of Saudi Arabia

Viungo vya Nje