Nenda kwa yaliyomo

Saumu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Swaumu)
Sura ya Buddha aliyekonda kutokana na juhudi zake kali. Gandhara, karne ya 2 au ya 3 BK, British Museum.
Mwisho wa mfungo mskitini.

Saumu (kutoka neno la Kiarabu صوم, sawm, linalotokana na Kiaramu ܨܘܡܐ, ṣawmā. Maana yake ni "kujikatalia", kama neno la Kiebrania tsom)[1] ni tendo la kujinyima chakula kwa sababu za kidini, ili kuweka roho huru kutoka utawala wa mwili wake, iweze kuinuka kwa Mungu na kutafakari kwa urahisi zaidi.

Kuna pia malengo mengine ya saumu, kama vile kushikamana na mafukara.

Katika dini

[hariri | hariri chanzo]

Karibu dini zote zinafundisha umuhimu wa saumu, lakini namna ya kufunga chakula ni tofauti.

Uyahudi, madhehebu mengi ya Ukristo na hasa Uislamu vina siku maalumu za toba zinazodai kufunga.

Yesu, aliyefunga jangwani siku arubaini mfululizo, aliwaelekeza wafuasi wake hasa namna ya kufunga, akiwadai wasijitafutie sifa kwa binadamu wenzao.

Katika Matendo ya Mitume tunaweza kusoma juu ya mafungo yaliyoendana na sala katika jumuia za kwanza za Kanisa.

Matendo ya toba yanazingatiwa bado hasa na watawa, kwa namna ya pekee wamonaki.

Waislamu wanapaswa kufunga chakula na kinywaji, yakiwemo maji, kuanzia alfajiri hadi magharibi mwezi mzima wa Ramadhani. Saumu za sunna ni saumu yoyote ambayo si ya lazima, ila mtu anaifunga ili kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.

Saumu ina fadhila kubwa sana, na thawabu nyingi mno, tena maradufu, na kwa hakika Mwenyezi Mungu ameinasibisha saumu kwake yeye kwa ajili ya kuipa utukufu na kuitukuza. Katika Hadithi Al-Qudsy iliyopokewa na swahaba Abu Hurayrah, anasema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu: “kila tendo la mwanadamu huongezwa malipo ya wema wake mara kumi ya mfano wa jema hilo alilolitenda mpaka hufikia kuongezwa (huku kwa malipo ya wema huo) hadi nyogeza mara sabiini. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Isipokuwa saumu, kwani hiyo saumu ni yangu mimi, na mimi ndiye mwenye kutoa malipo yake; (mja wangu) anaacha matamanio yake na chakula chake kwa ajili yangu. Katika kufunga saumu kuna furaha mbili: furaha (ya kwanza) ni pale anapofungua saumu aliyefunga, na furaha (ya pili) ni wakati (aliyefunga) atakapokutana na Mola wake. Na harufu inayotoka kwenye kinywa cha aliyefunga ni nzuri sana mbele ya Mwenyezi Mungu kushinda harufu ya miski”.[Imepokewa na Bukhari na Muslim.]<[2]

Baadhi ya fadhila za saumu katika Uislamu: "Asema Mwenyezi Mungu: Enyi mloamini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andkikwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kucha mungu.(Mfunge) siku maalumu za kuhisabika.na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimiza hisabu katika siku nyingine. Na wale wasio weza watoe fidiya kwa kumlisha masikini na atakaye fanya wema kwa kujitolea, Basi ni bora kwake na Mkifunga ni bora kwenu kama mnajua". (Al-Baqarah- Aya 183: 185)[3]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.