Nenda kwa yaliyomo

Anno Domini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Anno Domini (maneno ya Kilatini yanayomaanisha: "Mwaka wa Bwana"; kifupi: AD au A.D.) ni namna ya kutaja miaka katika kalenda ama Kalenda ya Gregori au Kalenda ya Juliasi.

Jina kamili ni "Anno Domini Nostri Jesu Christi" (Mwaka wa Bwana wetu Yesu Kristo) likirejea idadi ya miaka tangu kuzaliwa kwake Yesu Kristo.

Katika lugha ya Kiingereza ni njia ya kawaida ya kutaja miaka kama "AD" (ambayo ni sawa na matumizi ya BK) au "BC" yaani "before Christ" (tazama KK); ni pia kawaida katika maandiko ya kihistoria yanayotumia lugha ya Kilatini.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Anno Domini kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.