Muharram

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Muharram (Kiarabu: محرم ) ni mwezi wa kwanza katika kalenda ya Kiislamu. Ni kati ya miezi minne mitakatifu ya mwaka. Jina la mwezi limetokana na neno "haram" yaani "mwiko" au "kukatazwa" kwa maana ya kwamba vita haitakiwi mwezi huu.

Siku ya kwanza wa Muharram ni Mwaka Mpya wa Kiislamu.

Sikukuu ya Ashura iko mnamo tar. 10 Muharram. Hasa Waislamu Washia hukumbuka kifo cha Hussein ibn Ali (mjukuu wa Mtume Muhammad anayeheshimiwa kama Imamu wa Washia) kwenye mapigano ya Kerbela.

Kwa jumla Washia wanaangalia Muharram kama mwezi wa huzuni[1] na katika mazingira penye Washia wengi kuna mikutano mingi ya kidini ambako historia ya Ashura na kifo cha Hussein inakumbukwa kuanzia siku ya kwanza hadi ya kumi ambayo ni Ashura.

Kati ya Wasunni siku ya Ashurah inatazamiwa kama siku ya saumu hasa.[2].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Ibada za Mwezi wa Muharram, tovuti ya Kishia imamswadiq.com ya 2016, iliangaliwa Septemba 2018
  2. Fadhila Za Mwezi Wa Al-Muharram, Siku Ya 'Aashuraa Na Bid'ah Zake, mkusanyiko wa hadith kuhusu saumu ya Muharram, tovuti ya Kisunni ya alhidaaya.com, iliangaliwa Setemba 2018