Fatimah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Fatimah bint Muhammad (606 Makka - 632 BK au 11 BH Madina) (ajulikana pia kama Fatimah Zahra - فاطمة الزهراء) alikuwa binti wa Mtume Muhammad aliyezaa wajukuu wake wa pekee.

Wasunni huhesabu mabinti wanne lakini Washia humtazama kama binti wa pekee wa mtume.

Hakuna uhakika juu ya tarehe ya kuzaliwa kwake kulitokea kati ya 606 na 615; waandishi Wasunni wengine husema alizaliwa katika mwaka wa kutengenezwa kwa Kaaba yaani miaka mitano kabla ya ufunuo wa kwanza; wengine hudai kulitokea mwaka wa ufunuo na waandishi Washia mara nyingi husema alizaliwa miaka mitano baada ya ufunuo.

Alipofika umri wa kubalehe aliolewa na Ali ibn Abi Talib. Alikuwa mtoto wa pekee wa mtume aliyezaa watoto walioishi kuwa watu wazima. Kuna wavulana wawili na mabinti wanaokumbukwa:

Fatimah aliongozana na Muhammad alipofanya hijra kwenda Madina mwaka 622. Mtume alipogonjeka alimtunza hadi mauti. Baada ya kifo cha mtume alisimama upande wa Ali dhidi ya Abu Bakr aliyekuwa khalifa wa kwanza. Aligombana naye pia kuhusu urithi wake kutoka mtume. Abu Bakrs alipokataa kumpatia urithi alichodai alikataa kusema naye tena.

Fatimah aheshimiwa sana kati ya Waislamu hasa na Washia.