Nenda kwa yaliyomo

Hijra

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya

Uislamu

Imani na ibada zake

Umoja wa Mungu
Manabii
Misahafu
Malaika
Uteule
Kiyama
Nguzo za Kiislamu
Shahada Swalah Saumu
Hija Zaka

Waislamu muhimu

Muhammad

Abu Bakr Ali
Ukoo wa Muhammad
Maswahaba wa Muhammad
Mitume na Manabii katika Uislamu

Maandiko na Sheria

Azif Qur'an Sunnah Hadithi
Wasifu wa Muhammad
Sharia
Elimu ya Sheria za Kiislamu Kalam

Historia ya Uislamu

Historia
Sunni Shi'a Kharijiya Rashidun Ukhalifa Maimamu

Tamaduni za Kiislamu

Shule Madrasa
Tauhidi Falsafa Maadili
Sayansi
Sanaa Ujenzi Miji
Kalenda Sikukuu
Wanawake
Viongozi Siasa
Uchumi
Umma Itikadi mpya Sufii

Tazama pia

Uislamu na dini nyingine
Hofu ya Uislamu

Hijra (هجرة) ni neno la Kiarabu linalomaanisha tendo la Mtume Muhammad la kutoka Makka na kuhamia Madina mwaka 622 BK. Mwaka huo umekuwa tarehe ya kuanzisha kalenda ya Kiislamu ambayo miaka yake huhesabu miaka baada ya hijra.

Maana asili ya neno lenyewe ni "kuachana" au "kutengana", kutokana na historia ya Muhammad limechukua pia maana ya "kukimbilia" au "kuhamia".

Historia ya Hijra

[hariri | hariri chanzo]

Muhammad alianza kuhubiri habari za Kurani na za Uislamu katika mji wa Makka alipozaliwa na kuishi. Lakini hakupata wafuasi wengi. Kinyume chake kabila lake yeye mwenyewe la Wakuraishi walimchukia na kumtesa kwani viongozi waliogopa ataharibu biashara kubwa iliyoletwa na Kaaba iliyokuwa kama hekalu ya kidini mjini.

Hivyo Muhammad aliondoka Makka pamoja na babake mkubwa Abu Bakr; wafuasi wake kama 70 waliwahi kuondoka Makka siku zilizotangulia. Wote walipokelewa na watu wa Madina mji wa jirani.

Hapo Madina Muhammad akawa kiongozi aliyekubaliwa na watu wengi katika miaka iliyofuata aliunganisha Waarabu katika Uislamu mwishowe akarudi Makka ambako Wakuraishi walipaswa kumkubali yeye na dini ya Usilamu.

Katika kumbukumbu ya Waislamu wa kwanza tendo la hijra lilikuwa jambo muhimu sana. Sura za Kurani zilipokusanywa kila moja imeandikwa kama imepatikana kabla au baada ya hijra. Kila sura inaonyesha chini ya kichwa chake maneno ama (imeteremka Makka) au (imeteremka Madina).

Pia hesabu ya miaka ilianzishwa wakati wa khalifa wa pili Umar ikihesabu kuanzia tarehe ile ya kuhamia kwake Muhammad Madina.