Miaka baada ya hijra

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Miaka baada ya Hijra ni hesabu ya miaka katika kalenda ya Kiislamu.

Hesabu hii ilianzishwa miaka 17 baada ya tukio lenyewe (638 BK) kufuatana na azimio la Khalifa Umar ibn al-Khattab.

Waarabu waliwahi kuwa na kalenda iliyotumia mwendo wa mwezi lakini hawakuhesabu miaka. Kila mwaka ulitajwa kutokana na tukio fulani. Mwaka wa kuzaliwa kwake Mtume Muhammad hujulikana "Mwaka wa Tembo" kwa sababu mwaka ule Makka ilishambuliwa na jeshi la Waethiopia lililokuwa na tembo wa kijeshi.

Hata baada ya Muhammad desturi hii iliendelea. Mwaka wa Hijra wenyewe uliitwa "Mwaka wa kukubaliwa kwa safari," mwaka uliofuata "Mwaka vita ilipoamriwa," n.k.

Wakati wa Khalifa Umar ilionekana haja ya kuwa na hesabu inayoeleweka zaidi, hivyo hesabu ya Hijra ikachaguliwa.

Hesabu ya Kiarabu na Hesabu ya Kiajemi[hariri | hariri chanzo]

Waarabu Waislamu waliendelea kuhesabu miaka ya mwezi ya siku 29 au 30 kufuatana na kuonekana halisi kwa mwezi.

Hivyo miaka ya Kiislamu ina jumla ya siku takriban 354. Mwaka huo wa Kiislamu una siku 11 pungufu kuliko siku zile 365 za mwaka wa jua katika kalenda ya Kikristo. Mwaka 2006 BK ni 1427 BH (baada ya Hijra).

Uajemi hutumia hesabu ya miaka ya Hijra pamoja na mwaka wa jua. Hivyo mwanzo wa 2006 BK huko Uajemi ni mwaka 1384 BH (baada ya Hijra).

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.