Nenda kwa yaliyomo

Umar ibn al-Khattab

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Umar ibn al-Khattab (Kar.: عمر بن الخطاب) (mn. 5847 Novemba 644) alikuwa khalifa wa pili wa Uislamu. Alitawala baada ya Abu Bakr kati ya 634 hadi 644.

Umar alizaliwa kati ya Wakuraish wa Makka. Anasemekana ya kuwa awali alimchukia Muhammad na mahubiri yake lakini alivutwa na uzuri wa sura ya 20 katika Kurani akawa Muislamu. Akaongozana na mtume wakati wa hijra mwaka 622 akawa mshauri wake katika mambo ya siasa na vita.

Mwaka 625 binti yake Hafsah aliolewa na Muhammmad.

Abu Bakr aliyekuwa khalifa wa kwanza alimteua Umar amfuate akathebitishwa 634.

Umar aliuawa 644 na mtumwa Mwajemi mjini Madina. Alifuatwa na Uthman ibn Affan.

Uenezaji wa Uislamu[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa uongozi wa Umar eneo la Waarabu likakua sana. Jeshi zilitwaa Mesopotamia na Uajemi. Milki ya Uajemi iliporomoka kabisa baada ya ushindi wa Waislamu mwaka 642. Majimbo ya Palestina, Syria, Misri na Afrika ya Kaskazini yalitwaliwa na Bizanti lakini milki hii ilifaulu kujitetea katika eneo lililopungukiwa.

Yerusalemu ikatwaliwa mwaka 637; kwa jumla Waislamu waliheshimu makanisa ya Wakristo ila tu walianzisha msikiti ya Al Aqsa kwenye mlima wa hekalu.

Kwenye Bara Arabu aliamuru kufukuzwa kwa Waarabu Wakristo na Wayahudi wa Najran na Khaybar wasiopokea Uislamu.

Mwaka 639 alianzisha # Kalenda ya Kiislamu kwa kuagiza hesabu mpya ya miaka kuanzia hijra.