Ahlul-kisaa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ahlul-Kisaa (kwa Kiarabu: أَهْل ٱلْكِسَاء, ʾAhl al-Kisāʾ), au watu wa Cloak, ni mtume Muhammad; binti yake Fatimah; binamu yake na mkwe wake Ali; na wajukuu wake wawili Hassan na Huseyn.

Pia huitwa Aal al-Aba (Kiarabu: آل ٱلْعَبَاء ʾĀl al-ʿAbāʾ) na katika Panj-Tan ya Kiajemi (Kiajemi: پنج تن), maana yake ni 'Watano'. Asili ya imani hii inapatikana katika Hadith ya Tukio la Kishamia/Kujifunika shuka na Hadith ya Mubahala. Hadith hii imethibitishwa na Waislamu wa Shia na Sunni, hata hivyo Wasunni wengi wanatetea tafsiri tofauti.

Na ni moja ya misingi ya dhana ya Shia ya uimamu, ambayo inasema kwamba kizazi cha binti muhammad kina uongozi maalum wa kiroho wa kiungu juu ya jamii ya Waislamu. Ahal Kisa, pamoja na kizazi chao, Maimamu, wanaunda ufafanuzi wa Shia wa Ahl al-Bayt, "Watu wa Nyumba," au familia ya mtume Muhammad.

Matawi matatu makubwa ya Uislamu wa Shia yanatofautiana juu ya asili ya Ahal-Kisa na Maimamu. Matawi mawili makubwa, Shia mithnaashariya na Ismailia, wanachukulia kuwa hao watano wapo katika hali ya utakaso au kutofanya makosa: imani inayotoka katika Aya ya Utakaso katika Qur'an.

Kwa upande mwingine, tawi la tatu, Zaidia, linawaona tu kama viongozi wa kisiasa wenye wajibu wa kuongoza uasi dhidi ya watawala wafisadi na serikali.

Hadith ya kishamia[hariri | hariri chanzo]

Kwa Kiarabu ( حديث الكساء Hadith-e-Kisa) inahusu Ahal-Kisa/ watu wa kishamia. Hadithi ni maelezo ya tukio ambalo mtume Muhammad aliwakusanya Hassan, Huseyn, Ali, na Fatimah chini ya shuka/kishamia chake. Hii inajulikana katika hadithi kadhaa, ikiwa ni pamoja na ndani ya Sahih Muslim, ambayo Muhammad amenukuliwa akisema Ahl al-Bayt, au watu wa Nyumba, kutoka sehemu ya pili ya Aya ya Utakaso (ayat ul-tahir).

Hadithi hii ni muhimu kwa imani za Kishia. Kwa Shia, ni msingi wa mafundisho kwamba kiongozi wa Waislamu anapaswa kutakaswa (kwa mujibu wa Qur'an 33:33) na kutoka kwenye mstari huo wa moja kwa moja wa kizazi cha Muhammad kupitia Fatimah na Ali ambavyo vimetakaswa na Mungu. Pia hutumika kama mafundisho mengi ya Shia kwamba mlolongo huu wa uzao ni, safi, na hauna dhambi (ma'suum).

Hadith hii inaonyesha kwamba Muhammad, Fatima, Ali, Hasan, na Husein ndio wanachama pekee wa Ahl al-Bayt.

Waislamu wa Sunni pia wanakubali umuhimu wa kiroho wa tukio la utakaso kama ilivyotukuka ndani ya Qur'an na kufafanuliwa na Hadith Sahiih, lakini hawaunganishi na mamlaka ya kisiasa ambayo Waislamu wa Shia huyatoa kutoka kwa imani hii.

Hadithi inayohusishwa na ripoti za A'isha

...........kwamba Mtume wa Allah alitoka asubuhi moja akiwa amejifunika shuka lililofumwa na manyoya ya ngamia mweusi ambalo ailikuja Hasan ibn Ali. Akamfunika chini yake, akaja Husein, naye akafunikis chini yake pamoja na Hasan. Kisha akaja Fatima naye akamchukua chini yake, kisha akaja Ali na yeye pia akamchukua chini yake na kisha akasema: Mwenyezi Mungu anataka kuondoa uchafu wowote kutoka kwenu,na kuwatakasa enyi watu wa nyumba yangu"

Sunni huwa na mtazamo huu kua ni Sahih na wameijumuisha katika Sahih Muslim.

Muhtasari wa hoja[hariri | hariri chanzo]

Muktadha[hariri | hariri chanzo]

Baadhi ya wanazuoni wa Kisunni wanaamini kwamba wake wa mtume Muhammad walijumuishwa katika sehemu ya pili ya aya ya 33:33, kwa kuwa walishatajwa mwanzoni mwa aya ya 33:33. Wanakataa dhana kwamba mwisho wa aya hii utakuwa ni baraka ya kusimama peke yake, iliyomaanisha tu kwa Muhammad, Ali, Fatima, Hasan, na Husein, kama walivyo katika akili muktadha wa aya hii kwa ujumla na ule unaoitangulia.

Sunni wengi wangekubali hadith ya Sahih na kukubaliana na Shia kwamba upendeleo maalum unatolewa kwa watu watano.

Hoja ya shia ni kwamba aya yenyewe inasema "tu," ikimaanisha kwamba baraka ya sifa hii ni ya pekee kwa kikundi kimoja na si wake zake, yaani Mungu anataka kuondoa uchafu kutoka kwa wewe "tu" , "Enyi watu wa Nyumba yungu", na si kutoka kwa mtu mwingine yeyote, na hii ndiyo sababu amri sita za mistari mingine ndio zimetolewa kwaajili ya wake zake,  kwa sababu hawajalindwa na ni lazima kwao wachukue hatua ipasavyo; "watu wa nyumba ya nmtume", kwa upande mwingine, hawahitaji maagizo kama hayo. Waislamu wa Shia pia wanasema kwamba matamshi hayo yanabadilika na kuwa sauti ya kiume katika sehemu ya mwisho ya aya hiyo ambapo ilikuwa ya kabla ya hapo.

Jinsia[hariri | hariri chanzo]

Shia pia wanasema kuwa sehemu ya kwanza ya aya hii inazungumzia mtu au kikundi katika jinsia ya kike, wakati sehemu ya pili inazungumzia jinsia ya kiume, ikimaanisha kwamba angalau mtu mmoja katika kikundi ni mwanamume.

Wilfred Madelung,ni Profesa kutoka Laudian wa somo la kiarabu asiyekua muislam katika Chuo Kikuu cha Oxford, alifanya uchunguzi ufuatao juu ya Aya ya Utakaso:

"Watu wa nyumba" ni nani? Kiwakilishi kinachowazungumzia ni katika wingi wa kiume, wakati sehemu iliyotangulia ya aya iko katika wingi wa kike. Mabadiliko haya ya kijinsia yamechangia dhahiri kuzaliwa kwa nadhalia mbalimbali za tabia ya hadithi, ikiambatanisha sehemu ya mwisho ya aya hii kwa watu watano wa kishamia (ahl al-kisā'): Muhammad, 'Ali, Fātima, Hasan na Husein."

Kwa mujibu wa Laura Veccia Vaglieri katika Encyclopaedia ya Uislamu.

Aya ya Ḳur'ān (33, 33) inasema: "Mungu anataka kuwaondoa uchafu, Enyi watu wa Nyumba" (Ahl al-bayt) tu.Aya zilizotangulia zina maelekezo kwa wake za Mtume, na ina vitenzi na viwakilishi katika wingi wa kike; lakini katika aya hii, kuelekezwa kwa watu wa Nyumba, viwakilishi ni katika wingi wa kiume. Hivyo basi, imesemwa, sio tena swali la wake za Mtume, au miongoni mwao. Kwa hiyo, ina maana gani? Usemi wa Ahal-bayt unaweza kumaanisha "Familia ya Mtume" tu. Upendeleo uliotolewa na Mungu kwa mwisho (awali kabisa ulikiua wa kiroho, lakini baadaye sio hivyo tu) kwa kawaida uliwaongoza jamaa wote wa Muḥammad—wale walio karibu naye, wale walio katika matawi ya familia yake, na ni zaidi ya haya makundi ya jumuiya kama Anṣār, au jamii nzima kudai mahali/nafasi katika Ahl al-bayt. Lakini kuna hadithi iliyotolewa katika mila nyingi kulingana na ambayo Muḥammad alihifadhiwa chini ya hema lake (au chini ya kifuniko/shuka au chini ya aina ya hema), katika hali tofauti (ikiwa ni pamoja na tukio alipokuwa akijitayarisha kwa ajili ya mubahala (maapizano), wajukuu wake al-Ḥasan na al-Ḥusayn, binti yake Fāṭima na mkwe wake ʽAli; na hivyo ndivyo ilivyo kwa hawa watano ambao wamepewa jina la Ahl al-kisā' au "Watu wa kishamia" Juhudi zimefanywa kuwajumuisha wake wa mwisho wa Muḥammad; kwa ujumla hata hivyo idadi ya upendeleo ni maalumu kwa hawa watano.

Tukio la Mubahala/Maapizano[hariri | hariri chanzo]

Kwa mujibu wa makusanyo ya hadithi za Sunni, imesimuliwa kwamba katika mwaka wa 9 hadi mwaka wa 10 baada ya Hijra, mjumbe wa Kikristo wa Kiarabu kutoka Najran (kwa sasa kaskazini mwa Yemen na sehemu yake nchini Saudi Arabia) alikuja kwa Muhammad kubishana ni yupi kati ya pande hizo mbili zilizokosea katika mafundisho yake kuhusu Yesu (Quran 3:61). Muhammad alijitolea kufanya mila ya Kiarabu inayojulikana kama Mubahala/maapizano, ambapo kila upande unaopingana unapaswa kujifunika, na kwa pamoja pande zote zinamwomba Mungu kwa dhati kuangamiza na kusababisha laana juu ya upande unaosemaa uongo na familia zao. Muhammad, kuwathibitishia kwamba alikuwa ni mtume wa haki, alimleta binti yake Fatimah na wajukuu wake walionusurika, Hasan na Hussain, na Ali ibn Abi Talib na kurudi kwa Wakristo na akasema hii ni familia yangu (ahl) na kujifunika yeye na familia yake kwa kishamiya/shuka.

Shia wanaamini hadith hii halisi inathibitisha ni nani Qur'an inazungumzia wakati inataja Ahl al-Bayt ambayo inajumuisha Ali, Fatimah tu, na uzao wao. Wakati huohuo, vyanzo vingi vya Sunni vinakubaliana na imani ya Shia ikisema kwamba ni Ahl al-Kisa, Muhammad, binti yake Fatimah na wajukuu zake wawili, Hasan na Huseyn, na Ali ibn Abi Talib, walishiriki tukio hilo - hakuna hata mmoja wa wake zake, wajukuu wengine au wana-mkwe waliochaguliwa.

Mtazamo wa Shia[hariri | hariri chanzo]

Shia hua wanasherehekea tukio hili kama Eid-e Mubahala. Hadith hii inatoa historia ya "aya ya utakaso" au ayah al-tatheer kutoka surah Al-Ahzab katika Qur'an ambapo Mungu aliwataja wazi Ahlul-Bayt (33:33):

"Na kaeni majumbani mwenu, wala msijishauwe klwa majishauo ya kijahilia ya zamani. Na shikeni sala na toeni zakka, na mtiini M/mungu na mtume wake. Hakika M/mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi watu wa nyumba ya mtume, na kukusafisheni baarabbara".

Hadith hii inatokana na vyanzo tofauti kwa Fatimah, binti yake mtume Muhammad. Alisimulia kwamba mara tu baba yake alipomtembelea nyumbani kwake, alikuwa na homa na hakuwa akihisi vizuri, aliomba kisaa/kishamia cha Yemeni ambacho Fatimah alimletea na kuikunja karibu naye. Baadaye alijiunga katika ile nguo ya Yemeni na wajukuu wake Hassan na Husein, ambao walifuatwa na baba yao Ali, ambaye alikuwa binamu na mkwewe wa Muhammad.Hatimaye, Fatimah aliomba ruhusa ya kuingia kwenye nguo hiyo. Wakati wote watano walipoungana pamoja chini ya kishamia, mtumen Muhammad alisimulia Aya ya Qur'an 33:33 kwa wale walio chini ya kishamia kwamba wote watano kati yao wamechaguliwa, na akasema zaidi kwamba Mwenyezi Mungu anataka awaweke watu wote mbali na uchafu/maasi. Muhammad kisha akamwomba Mungu kuwatangaza wote watano kama Ahl al-Bayt wake na kuwaweka Mbali Najasat (uchafu).Katika ombi hilo, Mungu mara moja alimtuma malaila Jibril kumfunulia Muhammad kwamba wote watano walip chini ya kishamia ni wapenzi zaidi na wa karibu zaidi na Mungu na wao ni Tahir (safi zaidi) bila dalili zozote za uchafu.

Utendaji wa kisiasa[hariri | hariri chanzo]

Hadithi ya kishamia (hadith al kisaa)na aya ya utakaso ilitumiwa kwa nyakati tofauti na Ahlul -Bayt kudai imani yao kwa uongozi wa kisiasa na kiroho wa jamii ya Waislamu. Kwa mfano, kwenye mkusanyiko ambao uliitishwa baada ya kifo cha Umar mnamo mwaka 644 kumchagua khalifa, Ali alitoa hoja ifuatayo: "Je, kuna yeyote miongoni mwetu mbali na mimi mwenyewe kuhusu nani "aya ya utakaso" iliteremshwa?" Walipojibu "hapana" aliendelea:"Watu wa Nyumba (ahlul-bayt) wamejawa na fadhila nyingi, kwa maana Qur'an inasema: "Mwenyezi Mungu anataka kuondoa uchafu wote kutoka kwenu, Enyi watu wa Nyumba ya Mtume, na kukuwekeni huru kabisa na makosa." Kwa hiyo Mungu ametuondolea maovu yetu yote, ya nje na ya ndani, na kutuweka imara katika njia ya kweli na ya haki.

Mtazamo wa kisunni[hariri | hariri chanzo]

Baadhi ya wanazuoni wa Kisunni wanasema kwamba "aya ya utakaso" ilifunuliwa kuhusu watu watano: Muhammad, Ali, Fatimah, Hassan na Husein. Wengine wanashikilia kwamba "aya ya utakaso" haiwezi kutaja upungufu wa Maimamu kwa sababu mazingira ya aya hii yanahusiana na wake za mtume Muhammad (saww) na wana umuhimu pia, la sivyo angalau hawawezi kutengwa kutolewa katika jamii/watu wanaozungumziwa katika aya hiyo. Kama ingekuwa ni kuashiria Kutolewa/kutengwa, basi wake za Muhammad pia wangepaswa Kutengwa (wawe wahusika pekee wa moja kwa moja), imania mbayo wanazuoni wa Kisunni hawaishiki. Wanazuoni wa Kishia, hata hivyo, wanaamini katika Kutofanya makosa/ umaasumu wa mtume Muhammad. Ibn Kathir katika tafsir yake ya aya husika anasema "wanazuoni [wa Sunni] wamekubaliana kwa kauli moja kwamba [wake za mtume Muhammad] ndio sababu ya ufunuo katika aya hii, lakini wengine wanaweza kujumuishwa kwa njia ya jumla."

Hata hivyo, kwa mujibu wa mwanahistoria wa Sunni al-Tabari, neno ahl al-bayt linamaanisha 'Ali, Fatima, Hasan, na Husein. Kwa kuzingatia aya ya 33:33, L. Veccia Vaglieri katika Encyclopedia ya Uislamu aliandika:

.....aya zilizotangulia zina maelekezo kwa wake wa Muhammed, na kuna vitenzi na viwakilishi viko katika wingi wa kike; lakini katika aya hii, kuelekezwa kwa watu wa Nyumba, viwakilishi ni katika wingi wa kiume. Kwa hivyo, imesemwa, sio tena swali la wake wa Muhammed, au wao peke yao.... Usemi Ahl al-bayt unaweza kumaanisha tu "Familia ya Mtume".