Maria kutolewa hekaluni
Bikira Maria Kutolewa Hekaluni ni kumbukumbu ya liturujia inayoadhimishwa na Wakatoliki na Waorthodoksi tarehe 21 Novemba[1][2].
Msingi
[hariri | hariri chanzo]Adhimisho linatokana na habari ambayo haipatikani katika Agano Jipya, ila katika Injili ya Yakobo. Humo inasimuliwa kwamba wazazi wa Bikira Maria, Yohakimu na Ana, ambao hawakuwa na watoto, walipata ujumbe kutoka mbinguni kwamba watapata mtoto.
Kama shukrani ya kupata mtoto wa kike, akiwa bado mdogo walimleta katika Hekalu la Yerusalemu ili kumweka wakfu kwa Mungu[3].
Huko alibaki hadi alipotolewa kwa Yosefu.[3][4]
Kwa namna nyingine, inaaminika kwamba mwenyewe alijitoa mapema kwa Mwenyezi Mungu, yeye aliyejaa neema tangu kutungwa mimba kwa kukingiwa dhambi ya asili na atakayejaliwa kuwa Mama wa Mungu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu [5].
Asili
[hariri | hariri chanzo]Sikukuu ilianzishwa kuhusiana na kutabaruku Basilika jipya la Mtakatifu Maria, lililojengwa mwaka 543 na kaisari Justinian I karibu na mabaki ya Hekalu la Yerusalemu.[4]
Kutoka Ukristo wa mashariki sikukuu ilienea katika monasteri za Italia Kusini katika karne ya 9, ikaingia katika liturujia ya Papa wa Avignon mwaka 1372 kwa agizo la Papa Gregori XI.[6][7]
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Mchoro wa Bartolo di Fredi, 1360 hivi.
-
Mchoro mdogo wa Limbourg Brothers, 1415 hivi.
-
Mchoro wa Sano di Pietro, 1450 hivi.
-
Mchoro wa Fra Carnevale, 1467 hivi.
-
Mchoro wa Master of Wilten, karne ya 15.
-
Mchoro wa Hans Holbein the Elder, 1493.
-
Mchoro wa Cima da Conegliano circa 1500.
-
Mchoro wa Titian, 1535 hivi.
-
Picha takatifu ya Russia, karne ya 16.
-
Mchoro wa Alfonso Boschi, karne ya 17.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ Some but not all Eastern Rite churches reckon by the Julian calendar, in which this date falls 13 days later on December 4 of the Gregorian calendar.
- ↑ 3.0 3.1 "Peters, Sr. Danielle. "The Holy Land: In the Footsteps of Mary of Nazareth", Marian Library, University of Dayton". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-06-12. Iliwekwa mnamo 2016-10-14.
- ↑ 4.0 4.1 "Mauriello, Matthew R., "November 21: Presentation of Mary", Fairfield County Catholic, 1996". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-10-03. Iliwekwa mnamo 2016-10-14.
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/25200
- ↑ "The Saint Andrew Missal, with Sundays and Feasts," by Dom Gaspar LeFebvre, O.S.B., Saint Paul, MN: The E. M. Lohmann Co., 1952, p. 1684
- ↑ William E. Coleman, Ed. "Philippe de Mezieres' Campaign for the Feast of Mary's Presentation," Toronto: Pontifical Institute of Mediaeval Studies, 1981, pp. 3-4.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- The Entry of the Most Holy Mother of God into the Temple Orthodox Icon and Synaxarion
- Feast of the Presentation of the Blessed Virgin Mary - Catholic Encyclopedia article
- Foley O.F.M., Leonard. "Presentation of Mary",Saint of the Day, Lives, Lessons, and Feast, (revised by Pat McCloskey O.F.M.), Franciscan Media, ISBN 978-0-86716-887-7 Archived 4 Machi 2016 at the Wayback Machine.
- Butler, Alban. "The Presentation of the Blessed Virgin Mary", The Lives of the Fathers, Martyrs and Other Principal Saints, Vol. III Archived 8 Septemba 2016 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Maria kutolewa hekaluni kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |