Nenda kwa yaliyomo

Malaysia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Malesia)
Shirikisho la Malaysia
Malaysia
مليسيا (Jawi)
Kaulimbiu: Bersekutu Bertambah Mutu
("Umoja Huongeza Ubora")
Wimbo wa taifa: Negaraku ("Nchi Yangu")
Mahali pa Malaysia
Mji mkuu
na mkubwa
Kuala Lumpur
Lugha rasmiKimalay (Melayu)
Lugha ya taifaKiingereza
Kabila (2023)
Dini (2020)
  Mfalme
Ibrahim Iskandar
Anwar Ibrahim
  Uhuru wa Malaya
31 Agosti 1957
  Utawala wa Sarawak
22 Julai 1963
  Muungano wa Malaysia
16 Septemba 1963
Eneo
  Jumlakm2 330,803 (ya 67)
  Maji (asilimia)0.3%
Idadi ya watu
  Kadirio la 202434,564,810
  Msongamano101/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2025
  Jumla $1.470 trilioni
  Kwa kila mtu $43,470
PLT (Kawaida)Kadirio la 2025
  Jumla $444.98 bilioni (ya 35)
  Kwa kila mtu $13,140
HDI (2023) 0.819
- juu sana
Gini (2021)40.7
SarafuRinggit ya Malaysia (RM) (MYR)
Majira ya saaUTCUTC+8 (MST)
Msimbo wa simu+60
Jina la kikoa.my
Ramani ya Malaysia.

Malaysia, rasmi kama Shirikisho la Malaysia, ni nchi katika Asia ya Kusini-Mashariki, inayojumuisha Rasi ya Malay na sehemu ya kaskazini ya kisiwa cha Borneo, pamoja na visiwa vichache vidogo.Inapakana na Uthai kaskazini, Singapore kusini, Brunei na Indonesia mashariki. Mnamo 2024 Malaysia ina idadi ya watu takriban milioni 34, ikiwa ya 44 duniani. Jiji lake kubwa zaidi ni Kuala Lumpur, ambalo pia ni mji mkuu. Malaysia inajulikana kwa utofauti wake wa kitamaduni, rasilimali asili tajiri, na maendeleo ya haraka ya uchumi, ikifanya kuwa nchi muhimu katika Asia ya Kusini-mashariki. Kisiasa Malaysia ni shirikisho la majimbo 13 na maeneo ya shirikisho 3.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Nchi ilianzishwa mwaka 1963 wakati Shirikisho la Kimalay (kwa Kimalay: Persekutuan Tanah Melayu) liliungana na Singapur, Sabah na Sarawak ambazo awali zilikuwa chini ya Uingereza.

Hata hivyo Singapur iliondoka mwaka 1965 ikawa nchi ya pekee.

Majimbo ya Shirikisho

[hariri | hariri chanzo]

Malaysia ni Shirikisho la Kifalme. Tisa kati ya majimbo yake 13 ni sultani chini ya utaratibu wa kifalme na manne hufuata muundo wa jamhuri.

Majimbo ya shirikisho ni kama yafuatavyoː

Sultani tisa zinazoongozwa na Sultani pamoja na waziri mkuu anayechaguliwa na bunge la jimbo:

Majimbo manne chini ya gavana anayeteuliwa na serikali kuu na waziri mkuu anayechaguliwa na bunge la jimbo:

Maeneo matatu ya shirikisho:

Demografia

[hariri | hariri chanzo]

Wakazi ni mchanganyiko mkubwa, lakini Wamalay (50.1%) na wakazi asili wengine walio Waislamu wanapewa na katiba ya nchi nafasi ya pekee. Wachina ni 22.6%. Wahindi ni 7.3%

Lugha rasmi ni Kimalay, lakini zinatumika pia lugha nyingine 136.

Msikiti wa Kitaifa Kuala Lumpur

Dini rasmi ni Uislamu unaofuatwa na 61.3% za wakazi (wengi wakiwa Wasuni), wakati 19.8% ni Wabuddha, 9.2% ni Wakristo, 6.3% ni Wahindu, 1.3% ni wafuasi wa dini za Kichina (Ukonfusio na Utao).

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Malaysia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.