Akoliti
Mandhari
Akoliti (kwa Kiingereza "acolyte", kutoka Kigiriki ἀκόλουθος, akoluthos, yaani "msindikizaji") ni Mkristo anayemsaidia askofu, padri au shemasi anapoongoza ibada fulani[1].
Katika Kanisa la Kilatini
[hariri | hariri chanzo]Katika Kanisa la Kilatini tangu mwaka 1972, pamoja na usomaji, ni mojawapo kati ya huduma mbili za lazima[2] ambazo wale wote wanaojiandaa kupata daraja takatifu wazipate na kuzitekeleza kwa muda fulani.
Kati ya kazi muhimu za akoliti, mojawapo ni kuwagawia waamini wenzake sakramenti ya ekaristi[3].
Kuanzia mwaka 2021 wanawake pia wanaweza kupewa kazi hiyo, baada ya Papa Fransisko kurekebisha kanuni 230 ya Mkusanyo wa Sheria za Kanisa.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ General Instruction of the Roman Missal
- ↑ "Ministeria quaedam, II".
- ↑ General Instruction of the Roman Missal, no. 100
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- John N. Wall. A Dictionary for Episcopalians. Cambridge, MA: Cowley Publications, 2000.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Akoliti kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |